Nenda kwa yaliyomo

Busi Mhlongo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Busi Mhlongo (28 Oktoba, 194715 Juni, 2010 ), jina la kuzaliwa Victoria Busisiwe Mhlongo , alikuwa mwimbaji na mtunzi mahiri kutoka Inanda huko Natal, nchini Afrika Kusini. [1] [2]

Akitumia mitindo mbalimbali ya Afrika Kusini kama vile Mbaqanga, Maskanda, Marabi na Kizulu, ambapo aliunganisha na vipengele vya kisasa kutoka mitindo mbalimbali kama jazz, funk, rock, gospel, rap, opera, reggae na muziki wa Afrika Magharibi.[3]

Mnamo miaka ya 1960, alipitisha jina lake la kisanii la Vickie, Baadae alijulikana na Busi Mhlongo. Alianzisha sangoma, ambayo alisaidia katika katika muziki wake. [4]

Miaka ya 1970, Mhlongo alihamia London, baadae akarekodi na wasanii wengine wa Afrika Kusini waliokuwa wakiishi uhamishoni, kama vile Dudu Pukwana na Julian Bahula . Kufikia miaka ya 1980, alianza kutumbuiza kimataifa, aliigiza na wasanii wengine mashuhuri kama vile Salif Keita .

Kufikia miaka ya 1990, alianza kutoa kazi zake binafsi, na albamu yake ya kwanza ya Barbentu, ilitolewa mwaka 1993. Mwaka mmoja baadae, alijiunga na ziara ya nyumbani ya Hugh Masekela.

Mnamo 1995, Mhlongo alijiunga na Hugh Masekela katika tamasha la Afrika '95 huko London. Mnamo 1998, alitoa albamu yake ya pili ya Urban Zulu, ambayo ilivuma sana katika masoko mbalimbali duniani na inasemekana alitumia miezi kadhaa katika chati za Billboard World Music. [5] Aliendelea kutoa albamu kadhaa zaidi kama Freedom (2003), na ya mwisho Amakholwa kabla ya kifo chake kutokana na saratani ya matiti mnamo Juni 2010.

Maisha binafsi

[hariri | hariri chanzo]

Mhlongo alilelewa katika familia iliyopenda muziki katika kijiji cha Ohlange. Aliolewa na mpiga ngoma Early Mabuza, na baadae wakapata binti. [1] Kutokana na uhamisho wa Mhlongo, hakuweza kumlea binti yake wala kuhudhuria mazishi ya mumewe ambaye chanzo cha kifo chake ilikua mauaji.

Tuzo na uteuzi

[hariri | hariri chanzo]

Mhlongo aliteuliwa kuwania tuzo ya Grammy na akashinda tuzo tatu za Muziki za Afrika Kusini .

  1. 1.0 1.1 Tolsi, Niren (18 Juni 2010). "Subverting and owning maskanda". Mail and Guardian.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Harris, Craig. [Busi Mhlongo katika Allmusic "Biography: Busi Mhlongo"]. Allmusic. Iliwekwa mnamo 2 Mei 2010. {{cite web}}: Check |url= value (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Busisiwe Victoria Mhlongo | South African History Online". www.sahistory.org.za. Iliwekwa mnamo 2023-02-26.
  4. Bradshaw, Paul. "Busi Mhlongo – Urban Zulu & Queen of Maskanda 1947 -2010". Mondomix. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2 Novemba 2010. Iliwekwa mnamo 23 Januari 2012.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. "Freedom by Busi Mhlongo" (kwa Kiingereza (Canada)). Iliwekwa mnamo 5 Desemba 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Busi Mhlongo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.