Bungu-bahari

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bungu-bahari
Teredo navalis
Teredo navalis
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Mollusca (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Ngeli: Bivalvia (Wadudu)
Oda: Myida (Wadudu walio na mabawa yenye vigamba)
Familia ya juu: Pholadoidea
Lamarck, 1809
Ngazi za chini

Familia 2:

Bungu-bahari ni moluska wa baharini aina ya koambili wanaotoboa mbao kwenye maji ya chumvi. Hapo awali hii ilikuwa mbao zilizopelekwa hadi baharini, lakini siku hizi pia ni mbao za mashua na miundo katika bahari, kwa hivyo wanyama hao husababisha hasara kubwa. Katika Afrika ya Mashariki spishi za bungu-bahari kwa ujumla zimo katika familia mbili: Pholadidae na Teredinidae.

Spishi za Pholadidae zinaonekana kama koambili wa kawaida. Hutoboa matope ya sakafu ya bahari au miamba myororo au hata mbao. Huchimba kwa kugeuza makombe yao kama mfuo. Wanaishi ndani ya machimbo maisha yao mazima na kutoa tu mrija wa kufyonza maji yenye chembe za chakula.

Umbo la Teredinidae limebadilika kuwa kama minyoo wenye makombe madogo mawili upande wa mdomo ambayo hutumika kwa kutoboa ndani ya mbao. Moluska hao hula mbao pamoja na planktoni. Katika matamvua yao kuna bakteria zinazogeuza nitrojeni na kusaidia kumeng'enya selulosi ya mbao.

Spishi muhimu za Afrika ya Mashariki[hariri | hariri chanzo]

Pholadidae

  • Martesia striata

Teredinidae

  • Lyrodus pedicellatus
  • Teredo fulleri
  • Teredo navalis

Picha[hariri | hariri chanzo]