Buibui/Baibui


Page Module:Sidebar/styles.css has no content.
Buibui ama baibui ( , Arabic ʿabāyah, hasa katika Fasihi Kiarabu : عباءة ʿabā'ah ; wingi عبايات ʿabāyāt, عباءات ʿabā'āt ), wakati mwingine pia huitwa abaya, ni vazi jepesi, huru, refu na lenye kusitiri mwili wa mvaaji, kimsingi ni vazi linalofanana na joho, linalovaliwa na baadhi ya wanawake katika ulimwengu wa Kiislamu ikiwa ni pamoja na sehemu kubwa ya Mashariki ya Kati, Afrika Kaskazini, Afrika Mashariki na sehemu za Pembe ya Afrika . [1] Mabuibui za kitamaduni, kawaida huwa meusi na yanaweza kuwa mraba mkubwa wa kitambaa kilichofunikwa kutoka mabegani au kichwani au mtandio mrefu. Buibui hufunika mwili mzima isipokuwa kichwa (wakati mwingine), miguu, na mikono. Inaweza kuvaliwa na niqāb, barakoa la uso linalofunika uso wote isipokuwa macho. Baadhi ya wanawake pia huvaa glavu ndefu nyeusi, kwa hivyo mikono yao pia hufunikwa. Kwa kawaida, buibui huvaliwa na wanawake wanapotoka majumbani mwao au hata katika hafla maalum, kama vile arusini, sherehe za sikukuu za Kiislamu za Eid al-Fitr na Eid al-Adha, na pia wakati wa mwezi mtakatifu wa Kiislamu kama Ramadhani .
Mantiki
[hariri | hariri chanzo]Sababu ya kuvaa kwa wanawake buibui mara nyingi ni kutokana na aya ya Quran isemayo, "Ewe Mtume, waambie wake zako na binti zako, na wanawake waumini, wajifunike nguo legevu. Kwa hivyo watatambuliwa na hakuna madhara yatakayowapata" (Qur'an 33:59, iliyotafsiriwa na Ahmed Ali ). Nukuu hii mara nyingi hutumika kama maagizo kutoka kwa Mungu kuhusu kuvaa buibui.
Nchi
[hariri | hariri chanzo]Nje ya baadhi ya nchi kama vile Saudi Arabia, Iraq, Yemen, UAE, Qatar na Pakistan [2] buibui huvaliwa mno na wanawake Waislamu. Buibui pia huwa tafauti katika baadhi ya nchi. Katika nchi za Kiarabu ya Ghuba la Uajemi, huwa na rangi nyeusi.
Saudi Arabia
[hariri | hariri chanzo]Nchini Saudi Arabia, wanawake walitakiwa kujifunika wawapo hadharani. Hata hivyo, mnamo Machi 2018, Mwanamfalme Mohammad bin Salman alihoji kwamba wanawake wanaweza kujichagulia mavazi yao ya hadharani wao wenyewe, muradi yakidhi viwango fulani, aliposema, "Uamuzi umeachwa kabisa kwa wanawake kuamua ni aina gani ya mavazi ya heshima na staha wanayochagua kuyavaa".
Wanawake wa kigeni katika huduma nchini Saudi Arabia
[hariri | hariri chanzo]Rubani wa kijeshi wa Marekani Martha McSally aliyewakilishwa na Taasisi ya Rutherford katika kesi ya McSally dhidi ya Rumsfeld, kesi hio iliyofanikiwa mwaka wa 2001 dhidi ya Idara ya Ulinzi ya Marekani, ilipinga sera ya kijeshi iliyowataka wanajeshi wa Marekani na Uingereza walioko Saudi Arabia kuvaa mabuibui wanapotoka nje ya kambi nchini humo. [3]
Mwaka `wa 2002, Jenerali Tommy Franks, ambaye wakati huo alikuwa kiongozi wa maagizo makuu ya wanajeshi wa Marekani, alitangaza kwamba wanawake wa jeshi la Marekani hawatalazimika kamwe kuvaa mabuibui, ingawa "wangehimizwa" kufanya hivyo kama ishara ya kuheshimu desturi na mila za wenyeji. Akizungumzia mabadiliko hayo, msemaji wa maagizo makuu Kanali Rick Thomas alisema hayakufanywa kwa sababu ya kesi ya McSally lakini tayari yalikuwa "yamepitiwa" kabla ya kesi hiyo kuwasilishwa. McSally alikuwa akifanya kazi ya kubadili sera hiyo kwa miaka kadhaa na alikuwa amewasilisha kesi hiyo baada ya kutishiwa na mahakama ya kijeshi ikiwa hatatwii. [4]
Pia mwaka wa 2002, Bunge la Marekani lilipitisha sheria inayomkataza mtu yeyote katika jeshi "kuhitaji au kuwatia moyo wanawake wa kijeshi kuvaa mabuibui nchini Saudi Arabia au kutumia pesa za walipa kodi kuyainunua." [5] [6]
Falme za Kiarabu
[hariri | hariri chanzo]Mabuibui huvaliwa sana katika Falme za Kiarabu. Mara nyingi hutengenezwa kwa vitambara kama vile crêpe, georgette, na shifoni na rangi nyepesi kama kahawia na nyeupe zinazofaa hali ya hewa ya nchi hio.
Indonesia
[hariri | hariri chanzo]Mabuibui hujulikana kwa majina mbalimbali lakini hutumikia leng moja, ambalo ni kujistiri. Mitindo ya kisasa kwa kawaida ni kafeni, zilizokatwa kwa vitambaa vyepesi sana na vinavyotiririka kama vile crepe, georgette, na shifoni . Mitindo mingine inayojulikana ni buibui zilizo wazi mbele na abaya zilizofungwa mbele. Mitindo hutofautiana kutoka eneo hadi eneo: baadhi ya abaya zina ushonaji kwenye kitambaa cheusi, huku zingine zina rangi za kufunguka zina aina tofauti za kazi za kisanaa.
Marufuku ya Mabuibui katika shule za Ufaransa
[hariri | hariri chanzo]Ushawishi wa mitindo ya Magharibi katika miundo ya mabuibui
[hariri | hariri chanzo]Katikati ya karne ya 20, ushawishi wa mitindo ya ki-Magharibi yalianza kusambaa katika ulimwengu wa Kiarabu. Hii ilisababisha mabadiliko makubwa katika ushonaji wa mabuibui. Ingawa umbo la msingi lilibaki vile vile, vitambaa vipya kama vile hariri, shiifoni na lace vilianzishwa. Wabunifu walianza kujaribu rangi, mifumo, mikato na mitindo, wakichanganya vipengele vya kitamaduni na mitindo ya kisasa.
Gymshark na Leana Deeb walitoa mkusanyiko wa mazoezi ya viungo ikiwemo mabuibui.

Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Page Kigezo:Reflist/styles.css has no content.
- Uislamu na mavazi
- Aina za hijabu
Marejeleo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Yarwood, Doreen (1978). The Encyclopedia of World Costume. New York: Bonanza Books. uk. 9. ISBN 0-517-61943-1.
- ↑ "Shop Online for Best Deals on Fashion Abaya Hijab and More". abayahijabavenue.pk (kwa American English). 2024-06-15. Iliwekwa mnamo 2024-08-22.
- ↑ Vojdik, Valorie (Summer 2002). "The Invisibility of Gender in War". Duke Journal of Gender Law & Policy. 9: 261–270. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Machi 6, 2011.
{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Whitehead, John W. (2002). "No Abaya for McSally". Liberty Magazine. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Julai 14, 2020. Iliwekwa mnamo Aprili 22, 2020.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "H.R.4546 - Bob Stump National Defense Authorization Act for Fiscal Year 2003". United States Congress. Desemba 2, 2002. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Januari 8, 2020. Iliwekwa mnamo 12 Mei 2020.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ De Wind, Dorian (Februari 21, 2011). "Should our Servicewomen in Afghanistan Have to Wear Headscarves?". The Moderate Voice. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Aprili 29, 2011. Iliwekwa mnamo Julai 16, 2011.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Kaur-Jones, Priya. " Kubuni upya abaya ya Saudia ." BBC . 12 Mei 2011.
- Historia ya Abaya. " Historia ya Abaya ."
- Tovuti ya Kiislamu ya Quran. " ."
- Historia na Mageuzi ya Abaya