Nenda kwa yaliyomo

Bruno Foresti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Bruno Foresti (6 Mei 192326 Julai 2022) alikuwa mchungaji wa Kanisa Katoliki la Italia. Alikuwa askofu mzee zaidi wa Italia wakati wa kifo chake akiwa na umri wa miaka 99.

Foresti alizaliwa Tavernola Bergamasca, Italia, na alipewa upadrisho tarehe 7 Aprili 1946. Alipewa nafasi ya askofu msaidizi wa Jimbo la Modena-Nonantola tarehe 12 Desemba 1974 pamoja na kuwa Askofu wa jimbojina la Plestia, akapewa uaskofu rasmi tarehe 10 Januari 1975. Kisha aliteuliwa kuwa Askofu mkuu wa Jimbo la Modena-Nonantola tarehe 2 Aprili 1976.

Mwisho Foresti alikuwa askofu wa Jimbo la Brescia, na alistaafu kutoka nafasi hiyo tarehe 15 Desemba 1998.[1][2]

  1. Erlandson, Greg (Januari 6, 1989). "Pope calls family missionaries 'leaven of Church'". Pittsburgh Catholic. Iliwekwa mnamo Agosti 1, 2021.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Archbishop Bruno Foresti †". Catholic-Hierarchy.org. Iliwekwa mnamo 31 Julai 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.