Bounnhang Vorachith

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Bounnhang Vorachith (kwa Kilao: ບຸນຍັງ ວໍລະຈິດ; amezaliwa 15 Agosti 1937) ni mwanasiasa wa Laos ambaye amekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi cha Watu wa Lao (kiongozi de facto) na Rais wa Laos (mkuu wa nchi kisheria) tangu mwaka 2016.

Hapo awali aliwahi kuwa Naibu Waziri Mkuu kutoka 1996 hadi 2001, Waziri Mkuu kutoka 2001 hadi 2006, na Makamu wa Rais wa Laos kutoka 2006 hadi 2016.