Nenda kwa yaliyomo

Boris Bim-Bad

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Boris Mikhailovich Bim-Bad (28 Desemba 1941 – 1 Machi 2023) alikuwa mwalimu wa Umoja wa Kisovyeti na Urusi na mwanachama wa Chuo cha Elimu cha Urusi]]. Bim-Bad, alikuwa na shahada ya uzamivu wa elimu (EdD), alikuwa profesa na mwanachama wa Jumuiya ya Kimataifa ya Falsafa na Kosmolojia.

Bim-Bad alizaliwa kwenye familia ya Mikhail Isaakovich Bim-Bad (1901–1960). Mjomba wake ambaye ni Profesa Max Isaakovich Bim-Bad (1914–1996), alikuwa mwanzilishi na mkuu wa kwanza wa Idara ya Uchumi wa vifaa vya barabara vya Taasisi ya Magari huko Moscow.

Bim-Bad alihitimu katika Taasisi ya Ufundishaji ya Jimbo la Moscow na kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Urusi, baadaye kikabadilishwa kuwa Chuo Kikuu cha Chuo cha Elimu cha Urusi.

Kuanzia 2001 hadi 2002, alikuwa akiongoza kipindi cha mchezo cha I Know Everything! kwenye chaneli ya TV-6 . Kwa maoni yake, "ukanaji Mungu ni imani, lakini ni unyama".

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Boris Bim-Bad kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.