Bonde la Fergana

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani ya kijiografia ya Bonde la Fergana.

Bonde la Fergana ni bonde katika Asia ya Kati linaloenea mashariki mwa Uzbekistan, kusini mwa Kirgizia na Tajikistan kaskazini.

Bonde hilo linapata umuhimu wake likiwa eneo lenye maji na rutuba linaloweza kulisha watu wengi kiasi katika mazingira yabisi ya Asia ya Kati.

Jiografia na jiolojia[hariri | hariri chanzo]

Bonde la Fergana kwenye ramani ya kihistoria.

Bonde la Fergana linaenea baina ya milima ya Tienshan upande wa kaskazini na milima ya Alai kusini. Bonde hilo lina eneo la takriban kilomita za mraba 22,000, urefu wake ni kama km 300 na upana wake km 70. Bonde lina umbo la pembetatu lilipokea rutuba kutokana na mito inayotelemka kutoka milima ya karibu ambayo ni mito ya Naryn na Kara Darya inayoungana kuunda mto Syr Darya. [1]

Tabianchi[hariri | hariri chanzo]

Tabianchi ya bonde hilo ni kavu na ya joto. Mnamo Machi joto linafikia 20°C, kisha huongezeka kwa kasi hadi 35°C mnamo Juni, Julai na Agosti. Wakati wa miezi mitano ifuatayo mvua ni ya nadra, lakini huongezeka kuanzia Oktoba. Wakati wa miezi ya baridi halijoto hushuka hadi -20°C mnamo Desemba na Januari.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Tangu nyakati za kale lilikuwa mahali ambako watu wa makabila, mataifa na tamaduni mbalimbali walikutana na kuishi pamoja. Habari za historia ya bonde hilo zinaanzia zaidi ya miaka 2,300 iliyopita.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. grida.no Archived 28 Septemba 2011 at the Wayback Machine.: topography and hydrography of the Ferghana valley.

Vyanzo[hariri | hariri chanzo]

Na Vasily Bartold :

  • "Sart" Encyclopaedia of Islam Vol. IV SZ (Leiden & London) 1934
  • "Фергана" Работы по Исторической Географии (Moscow) 2002 pp527-539 (Pia inapatikana kwa Kiingereza katika Vol. II ya toleo la awali la Encyclopaedia of Islam )

Waandishi wengine:

  • Rahmon Nabiyev, Из История Кокандского Ханства (Феодальное Хозяйство Худояр-Хана), Tashkent, 1973
  • Beisembiev T.K. "Ta'rikh-i SHakhrukhi" kak istoricheskii istochnik. Alma Ata: Nauka, 1987. 200 p. Summaries in English and French.
  • S. Soodanbekov, Общественный и Государственный Строй Кокандского Ханства, Bishkek, 2000
  • Beisembiev T. K. Kokandskaia istoriografiia : Issledovanie po istochnikovedeniiu Srednei Azii XVIII-XIX vekov. Almaty, TOO "PrintS", 2009, 1263 pp., ISBN 9965-482-84-5.
  • Beisembiev T. "Annotated indices to the Kokand Chronicles". Tokyo: Research Institute for Languages and Cultures of Asia and Africa, Tokyo University of Foreign Studies. Studia Culturae Islamica. № 91, 2008, 889 pp., ISBN 978-4-86337-001-2.
  • Beisembiev T. "The Life of Alimqul: A Native Chronicle of Nineteenth Century Central Asia". Published 2003. Routledge (UK), 280 pages, ISBN 0-7007-1114-7.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Bonde la Fergana kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.