Nenda kwa yaliyomo

Bonaventura wa Barcelona

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu yake.

Bonaventura wa Barcelona (jina la awali: Miguel Bautista Gran; Riudoms, 24 Novemba 1620 - Roma, 11 Septemba 1684) alikuwa Mhispania ambaye, kisha kubaki mjane, mwaka 1640 alijiunga wa utawa wa Ndugu Wadogo Wareformati kama bradha kwa jina la Bonaventura.

Mwaka 1656 alikwenda kuishi upwekeni zaidi [1]. Mwaka 1658 alikubaliwa na kardinali Francesco Barberini kuhamia Roma akiwa na nia ya kueneza mtindo huo ili kuchochea bidii shirikani.

Bila kujali upinzani, alifaulu kuongea na Papa Aleksanda VII [2] akakubaliwa naye kwa hati Ecclesiae catholicae regimini ya tarehe 30 Agosti 1662 [2].

Wafuasi walitakiwa kutii viongozi wa shirika, nao walitakiwa kuanzisha nyumba za upwekeni katika kila kanda.[3] Kwa kuwa waliovutiwa waliongezeka haraka, ilibidi zianzishwe nyumba nyingi zaidi, hata mjini Roma, kwenye kanisa la San Sebastiano al Palatino, tarehe 12 Desemba 1677: konventi hiyo mpya ikawa kitovu cha Kirekebisho.

Mwanzilishi alihamia huko hadi alipofariki tarehe 11 Septemba 1684.[2]

Papa Pius X alimtangaza mwenye heri tarehe 21 Mei 1906.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe aliyofariki dunia [4].

  1. Raimondo Sbardella, DIP, vol. I (1974), col. 1509.
  2. 1 2 3 Raimondo Sbardella, DIP, vol. I (1974), col. 1511.
  3. Raimondo Sbardella, DIP, vol. VII (1983), col. 1764.
  4. Martyrologium Romanum
  • Guerrino Pelliccia e Giancarlo Rocca (curr.), Dizionario degli Istituti di Perfezione (DIP), 10 voll., Edizioni paoline, Milano 1974-2003.
  • Il martirologio romano. Riformato a norma dei decreti del Concilio ecumenico Vaticano II e promulgato da papa Giovanni Paolo II, LEV, Città del Vaticano 2004.
  • Congregatio de Causis Sanctorum, Index ac status causarum, Città del Vaticano 1999.
  • Filippo Caraffa e Giuseppe Morelli (curr.), Bibliotheca Sanctorum (BSS), 12 voll., Istituto Giovanni XXIII nella Pontificia Università Lateranense, Roma 1961-1969.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.