Bokator

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha ya Msaada wa watu wawili wanaotetea shambulio la simba katika hekalu la Sambor Prei Kuk huko Cambodia

Bokator ni mchezo wa mapigano wenye asili katika nchi ya Cambodia ulioanza karibu miaka elfu moja na mia saba iliyopita [1]. Wakati huo ulikuwa mchezo uliochezwa na wanajeshi na uliaminika kuwa ni sehemu ya Sanaa ya mapigano.

Mchezo huu unatumia mbinu mbalimbali za kimapigo, kama ngumi, mateke na hata silaha.

Kama ilivyo kwa michezo mingine ya kimapigano, mchezo huu hujumuisha baadhi ya miondoko ya wanyama kama simba ukiwa umekusanya zaidi ya mbinu elfu kumi za kimapigano.

Tofauti na michezo mingine ya mapambano ambayo wachezaji huvaa mikanda kulingana na rangi za kiwango chao na uwezo wa kupigana, mchezo huu wachezaji huvaa shingoni vitambaa vijulikanavyo kama krama ambavyo ndivyo hutumika kutofautisha kiwango cha mchezaji mmoja na mchezaji mwingine [2] na ili mchezaji apate krama ya rangi nyeusi, hana budi kujifunza zaidi ya mbinu elfu moja za mapigo katika mchezo huu.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. 10 Insane Martial Arts You've Never Heard Of (en-US). Listverse (2013-07-02). Iliwekwa mnamo 2020-02-23.
  2. Bokator (en-US). Black Belt Wiki. Iliwekwa mnamo 2020-02-23.
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Bokator kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.