Bodys Isek Kingelez
Bodys Isek Kingelez au Jean Baptiste (1948 – 14 Machi 2015) alikuwa mchongaji wa sanamu na msanii kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, anayejulikana kwa kutengeneza miundo ya miji ya kubuniwa iliyotengenezwa kwa kadibodi, karatasi, tepu na vifaa vingine vya kawaida.[1] Kazi zake zimewasilishwa katika maonyesho mengi duniani kote, yakiwemo maonyesho ya Centre Georges Pompidou huko Paris, Makumbusho ya Sanaa ya Kisasa huko New York, pamoja na documenta XI huko Kassel.[2]
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Kingelez alizaliwa akiwa wa kwanza kati ya ndugu tisa huko Kimbembele-Ihunga, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (ambayo wakati huo ilikuwa Kongo ya Ubelgiji).[2][3] Baada ya kuhitimu elimu ya sekondari, alihamia Kinshasa mwaka 1970.[3][4] Hadi mwaka 1977, alisoma kwa muda na kujikimu kimaisha kwa kufundisha shuleni.[3][4] Aliajiriwa na Makumbusho ya Taifa huko Kinshasa kama mrekebishaji wa kazi za sanaa, hasa katika ukarabati wa vinyago vya Kiafrika hadi mwaka 1985 ambapo alianza kujikita kikamilifu katika shughuli za uchongaji wa sanamu ambazo baadaye zilimfanya ajulikane.[5][1][2]
Katika kipindi cha maisha yake, hakuwa na wakala wa biashara ya sanaa wa kumwakilisha katika kazi zake.[1] Alifariki dunia mnamo mwaka 2015 kutokana na ugonjwa wa saratani.[2][3]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- 1 2 3 "At MoMA, a Genius Finally Gets His Due". Time. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2025-01-14. Iliwekwa mnamo 2026-01-19.
- 1 2 3 4 "L'artiste congolais Bodys Isek Kingelez est mort". Le Monde.fr. 17 Machi 2015. Iliwekwa mnamo 21 Novemba 2017 – kutoka Le Monde.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - 1 2 3 4 Smith, Roberta (31 Mei 2018). "Fantastical Cityscapes of Cardboard and Glue at MoMA". The New York Times.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - 1 2 Smee, Sebastian (23 Mei 2018). "Review - Everyone in New York will be talking about this artist soon" – kutoka www.washingtonpost.com.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Kries, Mateo; Klein, Amelie (2015). Making Africa A Continent of Contemporary Design. Vitra Design Museum. uk. 337. ISBN 9783931936525.
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Bodys Isek Kingelez kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |