Nenda kwa yaliyomo

Bodo (mchoraji)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Bodo ( mchoraji ))

Camille-Pierre Pambu Bodo (anajulikana kama Bodo; 1953 – 5 Machi 2015) alikuwa mchoraji na mchungaji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Aliishi mjini Kinshasa. Bodo alikuwa mmoja wa waanzilishi na watetezi wakuu wa Shule ya Zaire ya Uchoraji wa Kisasa. Kazi zake, pamoja na zile za wasanii wengine zinaonyesha kwa nguvu imani yao katika uwezo wao wa kuunda sanaa inayoweza kubadilisha historia.[1]

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Bodo alizaliwa mwaka 1953 na kulelewa mjini Mandu. Alimaliza elimu yake ya sekondari huko Mandu mwaka 1970 na kuhamia Kinshasa mwaka huohuo ili kushiriki katika maonyesho ya kihistoria ya Art Partout. Mwaka 1980 Bodo aliokoka na kuwa Mkristo akawa mchungaji wa Uinjilisti wa kimataifa ndani ya Kanisa la Kipentekoste akiwa na usadiki kuwa jambo hilo lingebadilisha maisha yake.[2][3]

  1. Magnin, André (2005). African Art Now: Masterpieces from the Jean Pigozzi Collection. London: Merrell. uk. 70.
  2. "Untitled, 2013". Paddle8. Iliwekwa mnamo 6 Novemba 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Grive, Mary. "Non-Western Part 2". Mary Grive Art F200X. Iliwekwa mnamo 6 Novemba 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Bodo (mchoraji) kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.