Mto Bloukrans (KwaZulu-Natal)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Shughuli za Bungee juu ya daraja la Bloukrans

Mto Bloukrans (KwaZulu-Natal) unaanzia Emangosini Njesuthi Drakensberg, eneo la KwaZulu-Natal, Afrika Kusini. Unaendelea upande wa kaskazini magharibi, unapita kijiji cha Frere, kisha unaungana na mto Tugela.

Mto na matawimto yake havina mabwawa, ingawa umwagiliaji unatokea katika maeneo ya juu.

Jina lina asili katika Kiholanzi "Blaauwekrans" (Kizulu: Msuluzi) kutokana na miamba yenye rangi ya buluu katika eneo hilo.[1]

Tawimto kubwa la Bloukrans ni mto Nyandu ambao una tawi la Sterkspruit. Matawi mengine ni mito midogo ya Ududuma, Umsobotshe na Ubhubhu.

Shamba la De Hoek linapatikana sehemu ya juu ya Bloukrans.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. du Plessis, E.J. (1973). Suid-Afrikaanse berg- en riviername. Tafelberg-uitgewers, Cape Town. ku. 204–205, 281, 307. ISBN 0-624-00273-X. 
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika Kusini bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mto Bloukrans (KwaZulu-Natal) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.