Bitchat
Bitchat ni programu ya kutuma ujumbe kwa njia fiche (faragha ama ya kificho) kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine iliyotengenezwa na Jack Dorsey, mwanzilishi mwenza wa Twitter (amabayo sasa inajulikana kwa jina X) na Block, Inc. Iliyotangazwa mnamo Julai 2025, Bitchat huwawezesha watumiaji kutuma ujumbe kupitia njia ya Bluetooth - Bluetooth Low Energy (BLE) bila kuhitaji muunganisho wa intaneti, huduma ya simu za mkononi, akaunti za watumiaji, au seva kuu . Bitchat pia hutumia itifaki ya Nostr inayotegemea intaneti kwa ajili ya mawasiliano ya kimataifa.
Muhtasari
[hariri | hariri chanzo]Bitchat hutumia usanifu mseto wa ujumbe uliosimbwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine, wenye tabaka mbili za usafiri zinazosaidiana na mtandao wa mesh wa Bluetooth na Nostr ili kusaidia mawasiliano bila ya internet na mawasaliano kupitia intaneti. Inafanya kazi kwa kutuma jumbe ama meseji kupitia Bluetooth kulingana na mfumo wa Itifaki unaojulikana kama Noise Protocol Framework , [1] [2] [3] [4] [5] kuwezesha vifaa vilivyo karibu kusambaza ujumbe bila kuhitaji muunganisho wa intaneti. [6] [2] [7] Watumiaji wanaweza kupiga gumzo ama kuchati kwenye chaneli ya ndani #mesh, na tangu toleo la 1.3.0, njia za eneo zinazotegemea Geohash zinapatikana kupitia Nostr, na kuruhusu watumiaji mtandaoni kupiga gumzo na watu walio karibu au wa kimataifa. [8] Ujumbe wa moja kwa moja kutoka mtumiaji mmoja kwenda mwengine hutumia usimbaji fiche wa mwanzo hadi mwisho ( end-to-end encryption), huku Bluetooth ikipendelewa ama kutumiwa kwanza na hivyo Nostr kutumiwa kama dharura ama mbadala endapo Bluetooth itashindwa kufanya kazi. Zaidi ya hayo, programu hii ina kitufe cha dharura ama hofu ambacho mtumiaji ataweza kukitumia kwa kubonyeza mara tatu na akifanya hivyo data zote ama taarifa zilizohifadhiwa zitafutika. [7] Jack Dorsey amesema programu hiyo inafanana na mifumo ya ujumbe ya IRC . [9]
Historia
[hariri | hariri chanzo]Dorsey aliitangaza Bitchat kwa mara ya kwanza kwenye X (zamani Twitter) mnamo tarehe 6 Julai 2025. [2] [3] Alichapisha nyaraka zinazoeleze kwa undani namna programu hii invyofanya kazi kwenye ukurasa wake wa GitHub akielezea usanifu wake huu wa kutokutegemea mifumo mikuu (ya kiserikali) na muundo wa usimbaji fiche . [1] [10] [7] Zaidi ya hayo, programu hii iliingia katika majaribio ya beta kupitia TestFlight, na kufikia kwa haraka kikomo chake cha watumiaji 10,000. [2] [3] [1] Muda mfupi baada ya kutolewa kwa majaribio hayo ya programu kwenye TestFlight, mtafiti wa usalama aligundua kuwa inawezekana kujiigiza yani kujifanya mtumiaji mwingine na kuwasiliana na anwani za mtumiaji fulani, yani mtu anaweza kijifanya mtu fulani kumbe sio. Baadaye Dorsey aliongeza kwenye ukurasa wake kuwa mradi huu wa Bitchat ni kazi inayoendelea, haikupokea ukaguzi wa usalama wa nje, na huenda isifikie malengo yake ya kiusalama. [11]
Matumizi
[hariri | hariri chanzo]Bitchat imeundwa kwa ajili ya mawasiliano thabiti kipindi ambacho mitandao tuliyoizoea haipatikani au imeathiriwa, kwa mfano wakati wa majanga ya asili au kukatika kwa Intaneti . <ref name="ct-july-07">Young, Martin (7 Julai 2025). "Jack Dorsey tests Bitchat — decentralized messaging without internet". Cointelegraph (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 9 Julai 2025. Iliwekwa mnamo 9 Julai 2025.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)Young, Martin (7 July 2025). "Jack Dorsey tests Bitchat — decentralized messaging without internet". Cointelegraph. Archived Pia huwezesha mawasiliano katika matukio makubwa kama vile sherehe za muziki bila kutegemea muunganisho wa Intaneti . [1] [3] Programu hii inashughulikia masuala ya udhibiti na ufuatiliaji na inaendana na programu zilizopo kabla yake kama FireChat na Bridgefy, ambazo zilitumiwa na waandamanaji wa demokrasia huko Hong Kong . [7] [3] [2]
Programu hii imeonesha kuwa imekuwa ikitumika sana na waandamanaji nchini Madagaska mnamo Septemba 2025, huku kampuni ikiripoti upakuaji elfu 70 ndani ya wiki moja kutoka nchini humo, ikilinganishwa na jumla ya upakuaji elfu 360 duniani kote ambao kampuni hiyo iliripoti kufikia mwishoni mwa Septemba. Pia ilitokea Nepal wakati wa maandamano yake mwezi huo huo, upakuaji 50,000 kutoka kwa watumiaji wa Nepal mnamo Septemba 8, 2025 pekee. Mnamo Januari 2026, kulikuwa na ripoti za ongezeko la upakuaji wa Bitchat nchini Uganda na Iran wakati wa kukatika kwa intaneti.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- 1 2 3 4 Cuthbertson 2025.
- 1 2 3 4 5 Sigalos 2025.
- 1 2 3 4 5 Silberling 2025.
- ↑ Crawley, Jamie (8 Julai 2025). "Jack Dorsey Unveils Bitchat: Offline, Encrypted Messaging Inspired by Bitcoin". CoinDesk (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 9 Julai 2025. Iliwekwa mnamo 9 Julai 2025.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Johnivan, J. R. (8 Julai 2025). "Twitter Co-Founder Launches Bitchat, a Security-Focused, Bluetooth Messaging App". TechRepublic (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 9 Julai 2025. Iliwekwa mnamo 9 Julai 2025.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Bonk 2025.
- 1 2 3 4 Weatherbed 2025.
- ↑ "bitchat 1.3.0". GitHub. permissionlesstech. 20 Agosti 2025. Iliwekwa mnamo 6 Januari 2026.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Young, Martin (7 Julai 2025). "Jack Dorsey tests Bitchat — decentralized messaging without internet". Cointelegraph (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 9 Julai 2025. Iliwekwa mnamo 9 Julai 2025.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Ropek 2025.
- ↑ Crawley, Jamie (8 Julai 2025). "Jack Dorsey Unveils Bitchat: Offline, Encrypted Messaging Inspired by Bitcoin". CoinDesk (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 9 Julai 2025. Iliwekwa mnamo 9 Julai 2025.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)