Nenda kwa yaliyomo

Bigwala

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bigwala (Ngoma ya Busoga)
Kikundi cha Wandere wakicheza Bigwala
Jina Bigwala
Jamii inayocheza Wabusoga
Eneo Mashariki mwa Uganda Kigezo:Flag icon/core
Aina Muziki na dansi ya kifalme ya kitamaduni
Dhumuni Sherehe za kifalme, maadhimisho ya kijamii, kuenzi mfalme na historia ya Busoga
Asili ya kihistoria Ilianza katika sherehe za kifalme kama vile kutawazwa na mazishi ya wafalme
Vyombo vya muziki Tarumbeta za malinga
Leo Inakaribia kutoweka; huchezwa mara chache katika hafla maalum, chini ya uangalizi wa wataalamu wachache waliobaki

Bigwala ni aina ya muziki wa sherehe na dansi ya Kitamaduni ya Ufalme wa Busoga ulioko nchini Uganda, inayozingatia matumizi ya tarumbeta zilizotengenezwa kwa mashada ya malinga .[1] Kwa kawaida, tarumbeta moja huanza peke yake, kisha kuunganishwa na zingine nne au zaidi ambazo hutengeneza melodi kwa kupiga kwa zamu. Kisha waimbaji hujiunga, na baadaye wacheza dansi ambao huzunguka wapiga ala huku wakicheza kwa kuyumbayumba.[1][2]

Hapo awali, Bigwala ilikuwa ikitumbuizwa wakati wa sherehe za kifalme kama vile upokeaji wa mfalme mpya na mazishi, lakini siku hizi imekuwa ikichezwa katika hafla za kijamii, japo kwa nadra. Kwa sasa, kuna wazee wanne tu waliobobea katika kutengeneza, kupiga, na kucheza Bigwala, lakini juhudi zao za kurithisha kizazi kijacho zimekwamishwa na ukosefu wa fedha.Bigwala huchangia umoja na utambulisho wa Wabusoga, huku mashairi yakisimulia historia ya Ufalme, yakilenga hasa mfalme ambaye ni ishara ya utambulisho wa Busoga, pamoja na kuzungumzia masuala ya kijamii.[1]

Godfrey Alibatya, aliyesaidia kuipeleka Bigwala kwenye orodha ya UNESCO, anasema kuwa "kupotea kwa Bigwala kunaweza kuchangia kudhoofika kwa utawala wa kifalme" na hatimaye kwa Ufalme wenyewe.[3]David Pier anaeleza kuwa Alibatya anasaidia kuihifadhi Bigwala licha ya kutotambuliwa sana na jamii, tofauti na urithi mwingi wa UNESCO ambao hupendwa sana na wenyeji.[4][5]

  1. 1 2 3 "Bigwala", UNESCO.org.
  2. ↑ "Bigwala | Singing Wells" (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-01-19.
  3. ↑ Pier , David G. (2015). "Marketing Ebigwala to UNESCO: Strategies and Outcomes", Ugandan Music in the Marketing Era: The Branded Arena. Springer. ISBN 9781137546975.
  4. ↑ Pier (2015).
  5. ↑ Jidovanu, Natalia (2019-03-29). "To Revive This Royal Music, Ugandans Had to Grow New Instruments". Atlas Obscura (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-01-19.