Big Daddy Kane
| Big Daddy Kane | |
|---|---|
Big Daddy Kane mnamo 2023 | |
| Taarifa za awali | |
| Jina la kuzaliwa | Antonio Hardy |
| Pia anajulikana kama | B.D.K., Dark Gable, King Asiatic Nobody's Equal, Blackanova, Count Macula |
| Amezaliwa | Septemba 10 1968 Brooklyn, New York City, U.S. |
| Aina ya muziki | Hip hop |
| Kazi yake |
|
| Miaka ya kazi | 1987–hadi sasa[1] |
| Juice Crew | |
Antonio Hardy (alizaliwa 10 Septemba, 1968) anajulikana zaidi kwa jina lake la kisanii kama Big Daddy Kane, ni rapa, mtayarishaji na mwigizaji kutoka nchini Marekani. Alianza kazi yake muziki mnamo mwaka wa 1986 kama mwanachama wa kundi la rap la Juice Crew. Anachukuliwa na wengi kuwa mmoja kati ya MC mwenye ushawishi mkubwa na ujuzi katika hip hop. Rolling Stone iliorodhesha wimbo wake "Ain't No Half-Steppin'" kama wa 25 kwenye orodha yake ya Nyimbo 50 Bora za Hip-Hop za Wakati Wote, na kumtaja kama "mtaalamu wa maneno katika enzi ya dhahabu ya rap na mwenye ushawishi mkubwa kwa kizazi cha ma-MC."
Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Antonio Hardy alizaliwa Septemba 10, 1968, huko Brooklyn.[2]
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Miaka ya 1980
[hariri | hariri chanzo]Akiwa sekondari, Kane alikutana na Mister Cee, ambaye baadaye alihusika sana katika kazi ya Kane kama DJ wake.[3] Mwaka wa 1984, Kane alifanya urafiki na Biz Markie, na alishiriki kuandika baadhi ya mashairi maarufu ya Biz.[4][5] Wawili hawa baadaye wakawa wanachama wa kikundi cha Queens kinachojulikana kama Juice Crew, kikundi kilichokuwa chini ya mtayarishaji maarufu Marley Marl. Kane alisaini mkataba na kampuni ya Cold Chillin' Records ya Tyrone Williams (meneja wa Marl) na Len Fichtelberg mwaka 1987 na alijitambulisha rasmi mwaka huohuo kupitia single ya inchi 12 iliyoitwa "Raw", ambayo ilipata umaarufu katika mitaa. Jina Big Daddy Kane lilitokana na mchanganyiko wa jina la Caine, mhusika wa David Carradine katika kipindi cha televisheni Kung Fu (1972–1975), na mhusika aliyeitwa "Big Daddy" aliyochezwa na Vincent Price kwenye filamu Beach Party (1963).[6]
Kane anajulikana kwa uwezo wake wa kuimba kwa kasi juu ya midundo kasi ya hip hop—licha ya hali yake ya kuwa na pumu,[4] anatambuliwa kama mmoja wa waanzilishi wa mbinu ya kurap kwa kasi. Mtindo wake wa mavazi unajulikana sana na uliweka mitindo kadhaa ya hip hop ya mwishoni mwa miaka ya 1980 na mapema miaka ya 1990 (nywele zilizochanwa juu kwa mtindo wa high-top (kibwenzi), suti za velour, na pete za vidole vinne). Backronym "King Asiatic Nobody's Equal" mara nyingi hutumika kumwelezea.
Alitoa albamu yake ya kwanza kupitia Cold Chillin' Records mwanzoni mwa kiangazi cha 1988 inayoitwa Long Live the Kane, iliyojumuisha wimbo maarufu "Ain't No Half Steppin'". Mwaka uliofuata, Kane alitoa albamu yake ya pili na iliyofanikiwa zaidi hadi sasa, It's a Big Daddy Thing, iliyojumuisha sampuli za kurudi kwenye mitindo ya miaka ya 1970 kama "Smooth Operator" na wimbo uliotayarishwa na Teddy Riley "I Get the Job Done", ambao uliingia kwenye orodha ya juu ya muziki wa R&B mwishoni mwa miaka ya 1980. Pia alishiriki na kutoa beti isiyosahaulika kwenye wimbo wa Marley Marl "The Symphony" ulioachiwa mwishoni mwa 1988, uliowajumuisha wanachama wa Juice Crew Craig G, Masta Ace, na Kool G Rap.
Diskografia
[hariri | hariri chanzo]Albamu
[hariri | hariri chanzo]- Long Live the Kane (1988)
- It's a Big Daddy Thing (1989)
- Taste of Chocolate (1990)
- Prince of Darkness (1991)
- Looks Like a Job For... (1993)
- Daddy's Home (1994)
- Veteranz' Day (1998)
Filmografia
[hariri | hariri chanzo]- 1993 Posse as "Father Time"[7]
- 1993 The Meteor Man kama "Pirate" [8]
- 2005 Dave Chappelle's Block Party kama Yeye.[9]
- 2007 Dead Heist kama Mwindaji[10]
- 2008 Love for Sale[11]
- 2009 Just Another Day kama Clay
- 2011 Budz House kama Keisha
- 2016 Exposed kama Jonathan "Black" Jones
- 2018 Law & Order: Special Victims Unit as Ray Wallis / "Four Stroke"
- 2024 ElemenTory kama Chris Cunningham
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Ursula, Melissa; Goldsmith, Dawn; J. Fonseca, Anthony (2018). Hip Hop around the World: An Encyclopedia [2 volumes]. ABC-CLIO. ISBN 978-0313357596. Iliwekwa mnamo Novemba 16, 2019.
{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Hitilafu ya kutaja: Invalid
<ref>tag; no text was provided for refs namedallmusic1 - ↑ Horowitz, Steven (Aprili 10, 2024). "Mister Cee, Big Daddy Kane's DJ and Notorious B.I.G.'s Producer, Dies at 57". Variety. Iliwekwa mnamo Aprili 10, 2024.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - 1 2 "Big Daddy Kane: Rap Like No Equal | Rappers Talk Hip Hop Beef & Old School Hip Hop". HipHop DX. Septemba 20, 2010. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Januari 21, 2012. Iliwekwa mnamo Mei 3, 2012.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Coleman, Brian, 2007, Check the Technique: Liner Notes for Hip-Hop Junkies. New York:Villard/Random House, uk. 47.
- ↑ "::Halftimeonline.net | Big Daddy Kane | Hip Hop Icon Series interview ::". Halftimeonline.net. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Machi 4, 2014. Iliwekwa mnamo Septemba 5, 2009.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Posse". IMDb. Mei 14, 1993. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Aprili 2, 2016.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "The Meteor Man". IMDb. Agosti 6, 1993. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Mei 11, 2018.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Dave Chappelle's Block Party". IMDb. Machi 3, 2006. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Mei 11, 2018.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Dead Heist". IMDb. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Januari 27, 2013.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Love for Sale". IMDb. Agosti 8, 2008. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Mei 11, 2018.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]