Nenda kwa yaliyomo

Bibiarusi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Arusi ya Yosefu na Maria.
Msichana na beberu mwenye pembe moja tu, aliyetazamwa kumaanisha ubikira wake.
Bango dhidi ya ukeketaji na ndoa ya kulazimishwa.

Bibiarusi (pia biarusi, biharusi, bibiharusi) ni jina ambalo mwanamke huitwa siku chache kabla na baada ya kufunga ndoa.

Katika Ukristo

[hariri | hariri chanzo]

Katika Ukristo (k. mf. Ufu 22:17) ni jina la Kanisa katika uhusiano wake na Yesu Kristo ulivyoelezwa na Mtume Paulo hasa katika Waraka kwa Waefeso (5:22-33). Mfano huo uliendelezwa na Mababu wa Kanisa, kama Ireneo wa Lyon na wengineo.

Hapo Yesu anatazamwa kama Adamu mpya, mkuu wa binadamu wote: kama vile kutoka ubavu wake akiwa usingizini aliumbwa Eva, vivyo hivyo kutoka ubavu wa Kristo uliotobolewa akiwa maiti msalabani (Yoh 19:31-35) lilitolewa Kanisa, bibiarusi wake, likiwakilishwa na maji na damu vilivyodokeza sakramenti za ubatizo na ekaristi zinazoliunda.