Betty Krosbi Mensah

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Betty Krosbi Mensah
Betty Krosbi Mensah
Betty Krosbi Mensah
Nchi Ghana
Kazi yake Mwana sayansi

Betty Nana Efua Krosbi (jina hili pia huandikwa Crosby[1] au Krosby[2] Mensah; alizaliwa Donkorkrom, Mkoa wa Mashariki, 29 Agosti 1980[3]) ni mwanamke mwanasiasa nchini Ghana na Mbunge wa jimbo la Afram Plains North katika eneo la Mashariki mwa Ghana. Yeye ni mwanachama wa chama cha National Democratic Congress.[4][5][6]

Maisha na Elimu[hariri | hariri chanzo]

Betty Krosbi Mensah ana shahada ya kwanza ya Utawala wa Biashara kutoka Chuo Kikuu cha Zenith,[7] na Diploma ya Juu ya Taifa (Higher National Diploma) katika fani ya Uhasibu kutoka Chuo Kikuu cha Kiufundi cha Koforidua.[8]

Kazi yake ya Siasa[hariri | hariri chanzo]

Kabla ya kuwa Mbunge, Mensah alikuwa Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Best Pat Ghana Limited kuanzia mwaka wa 2013 hadi mwaka 2016. Pia aliwahi kuwa Naibu Mratibu wa Pili wa Ajira kwa Vijana Kitaifa nchini humo kutoka mwaka 2009 hadi mwaka 2013. Mensah pia alikuwa Mratibu wa Jinsia na Maendeleo wa Chama cha Mikopo cha Ushirika cha Ghana kutoka mwaka 2003 hadi mwaka 2005.[9]

Mchakato wa Kugombea Ubunge[hariri | hariri chanzo]

Katika uchaguzi mkuu wa Ghana wa mwaka 2016 wa kugombea kiti cha Ubunge wa jimbo la Afram Plains, Betty alijizolea jumla ya kura 18,121 kati ya kura 23,606 zilizopigwa akiwa ni sawa na 78.44% na kumshinda Isaac Ofori-Koree wa chama cha New Patriotic Party, Cornelius Agbeku wa chama cha National Democratic Party na Micheal Ampontia wa Chama cha Convention People's Party na kushinda kiti katika Bunge la 7 la Jamhuri ya Ghana. Katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020,alimudu tena kutetea kiti chake katika Uwanda wa Kwahu Afram Kaskazini kwa kupata 18,543 ikiwa ni sawa na 67.8% ya jumla ya kura (27,986).[10][11]

Majukumu Bungeni[hariri | hariri chanzo]

Katika bunge la nane akiwa Mbunge ametumikia kama mjumbe katika Kamati ya Jinsia na Watoto na Kamati ya Afya ya Bunge hilo.[3]

Maisha binafsi[hariri | hariri chanzo]

Betty ameolewa na ana mtoto mmoja wa kike.[7] Yeye ni mtoto Krosbi Mensah, mbunge wa kwanza wa jimbo la Afram Plains.[12] Betty ni Mkristo wa Kanisa Katoliki.[3]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 11 Young And Beautiful Ghanaian Female MPs Who Are Inspiring Girls To Dream Big. web.archive.org (2018-10-25). Jalada kutoka ya awali juu ya 2018-10-25. Iliwekwa mnamo 2022-03-30.
  2. Mensah, Betty Nana Efua Krosby (en-US). Ghana MPS. Iliwekwa mnamo 2022-03-30.
  3. 3.0 3.1 3.2 Parliament of Ghana. www.parliament.gh. Iliwekwa mnamo 2022-03-30.
  4. Parliament of Ghana. www.parliament.gh. Iliwekwa mnamo 2022-03-30.
  5. Youth resist attempts to relocate ferry at Afram Plains (en). GhanaWeb (2017-11-28). Iliwekwa mnamo 2022-03-30.
  6. News Ghana. NDC Parliamentary Candidate makes women her prime target | News Ghana (en-US). https://newsghana.com.gh/. Iliwekwa mnamo 2022-03-30.
  7. 7.0 7.1 MPs (en-US). Ghana MPS. Iliwekwa mnamo 2022-03-31.
  8. ICT Dept. Office of Parliament, Ghana. Parliament of Ghana. www.parliament.gh. Iliwekwa mnamo 2022-03-31.
  9. Parliament of Ghana. www.parliament.gh. Iliwekwa mnamo 2022-03-31.
  10. Peace FM. 2020 Election - Afram Plains North Constituency Results. Ghana Elections - Peace FM. Iliwekwa mnamo 2022-03-31.
  11. MPs (en-US). Ghana MPS. Iliwekwa mnamo 2022-03-31.
  12. Ingia kwenye Facebook (sw). Facebook. Iliwekwa mnamo 2022-03-31.