Nenda kwa yaliyomo

Beth Wambūi Mūgo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Beth Wambūi Mūgo
AmezaliwaBeth Wambūi Mūgo
Uraiamkenya
Kazi yakemwanasiasa
Kazi maarufuSenator

Beth Wambūi Mūgo (alizaliwa 11 Julai 1939 katika kaunti ya Kiambu) ni mwanasiasa kutoka Kenya. Anahusiana na Chama cha Party of National Unity na alichaguliwa kuwakilisha Kata ya Dagoretti katika Bunge la Kitaifa la Kenya katika uchaguzi wa bunge wa mwaka 2007

Beth Mūgo amekuwa na kazi yenye mafanikio katika siasa. Alikuwa mbunge mwenza (nominated member) wa Seneti kati ya tarehe 21 Machi 2013 hadi 16 Julai 2017. Pia alikuwa mbunge wa Dagoretti kwa niaba ya Chama cha Party of National Unity. Alikuwa Naibu Waziri wa Elimu (nchini) kati ya mwaka 2006 na 2007. Kati ya Januari na Julai 2003, alikuwa Naibu Waziri wa Utalii.

Hivi sasa, yeye ni Seneta aliyechaguliwa (nominated Senator). Alianza kazi yake tarehe 31 Agosti 2017. Beth Mūgo pia ni mwanachama wa Chama cha Jubilee kuanzia Januari 2017. Mwisho, yeye ni mwanachama wa muungano wa Jubilee Alliance.

Kazi nyingine

[hariri | hariri chanzo]

Yeye ndiye mwanzilishi na Mwamini (Trustee) wa( The Beth Mūgo Cancer Foundation. Seneta Beth Mūgo) ana uzoefu mpana wa kibinafsi na wa kitaalamu katika masuala yanayohusiana na saratani. Wakati alipopatiwa wadhifa wa Waziri wa Afya ya Umma na Usafi wa Mazingira nchini Kenya, Seneta Mūgo aliongoza maendeleo ya Mkakati wa Kitaifa wa Kudhibiti Saratani (2011-2016), kupitishwa kwa Sheria ya Kuzuia na Kudhibiti Saratani (2012), na kuanzishwa kwa Taasisi ya Kitaifa ya Saratani ya Kenya. Pia alipanua mapambano yake dhidi ya saratani kote barani Afrika alipokuwa Mwenyekiti wa Bunge la Afrika na Mawaziri wa Afya dhidi ya Saratani ya Matiti, Kifua na Prostate (2012-2014).

    Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
    Je, unajua kitu kuhusu Beth Wambūi Mūgo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
    Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
    Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.