Bessus

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mchoro wake katika kanisa kuu la Ivrea, Italia.

Bessus (alifariki mwishoni mwa karne ya 3) ni kati ya askari wa jeshi la Roma ya Kale katika kikosi cha Thebe kilichoongozwa na Morisi Mtakatifu[1].

Kufuatana na mapokeo ya karne ya 4 kikosi hicho kilijumlisha wanajeshi Waafrika kutoka Misri ya kusini na Nubia waliotumwa Ulaya wakati wa Kaisari Maximiano wa Roma. Wengi wao walikuwa Wakristo. Katika mapokeo ya sanaa ya Kikristo walichorwa kama Waafrika weusi.

Huko Agaunum (leo Saint-Maurice-en-Valais), karibu na mto Rhone, katika eneo la Uswisi wa leo, walipewa amri ya kujiandaa kwa mapigano dhidi ya waasi na kabla ya mapigano kutoa sadaka kwa Kaisari aliyeheshimiwa kama mungu mmojawapo. Wakristo hao walikataa kutoa sadaka hiyo. Kaisari alipopata habari hii akakasirika akatoa amri kuua kila askari wa kumi katika kikosi. Wakristo walipoendelea kukataa amri ilirudiwa hatimaye karibu kikosi chote kiliuawa pamoja na kiongozi chake Morisi.

Bessus na wachache wengine walinusurika wakahubiri Injili kwenye milima ya Alpi. Bessus alifanya hivyo Italia Kaskazini Magharibi.

Bessus pamoja na kikosi chake waliheshimiwa mapema kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 10 Agosti[2] lakini pia 1 Desemba.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Henry Wace, A Dictionary of Christian Biography, Literature, Sects and Doctrines (1880), 439.
  2. https://catholicsaints.info/saint-bessus/

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Robert Hertz, "San Besso. Studio di un culto alpestre", in La preminenza della destra e altri saggi, Einaudi, Torino, 1994.
  • Hertz, Robert. "Saint Besse: a Study of an Alpine Cult". In Saints and their Cults: Studies in Religious Sociology, Folklore and History. Editor Stephen Wilson. Cambridge: Cambridge University Press, 55-100.
  • Marco Reis, "Il mistero di Besso - Tra Cogne e Campiglia le radici di un popolo", Lampi di Stampa, 2006.
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.