Nenda kwa yaliyomo

Bertrand de la Tour

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bertrand de La Tour

Bertrand de la Tour (anajulikana pia kama Bertrand de Turre; 1265? – 1332 au 1333) alikuwa mwanateolojia na kardinali wa Ufaransa wa shirika la Wafransisko.

Alizaliwa Camboulit, katika jimbo la zamani la Quercy, Ufaransa. Kuanzia mwaka 1312, alihudumu kama mtumishi wa kanda ya Aquitaine akawa mpinzani mkuu wa kundi la Wafransisko wa Kiroho.

Kati ya miaka 1317–1318, alifanya kazi za kidiplomasia kwa niaba ya Papa Yohane XXII pamoja na Bernard Gui. Baada ya kipindi hiki, alihusika katika kutathmini mafundisho ya Petro wa Yohane Olivi yaliyoshukiwa kuwa ya uzushi.[1]

Mwaka 1320, de la Tour aliteuliwa kuwa Askofu Mkuu wa Salerno na baadaye kuwa Kardinali wa San Vitale. Mwaka 1323, aliteuliwa kuwa kardinali askofu wa Tusculum.

Baada ya kuondolewa madarakani kwa Mikaeli wa Cesena mwaka 1328, de la Tour aliteuliwa na Papa Yohane XXII kuwa vika mkuu wa Shirika la Wafransisko.

Alijulikana kwa lakabu ya "Doctor famosus" (Daktari mashuhuri).[2]

  1. Patrick Nold (2003). Pope John XXII and his Franciscan Cardinal: Bertrand de la Tour and the Apostolic Poverty Controversy. Oxford.
  2. Moorman, John H. R. (1968). A History of the Franciscan Order from its Origins to the Year 1517 (kwa Kiingereza) (tol. la 1st). Oxford: Clarendon Press. ku. 321. ISBN 978-0819909213.
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.