Berkeli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Berkelium)

Berkeli (Berkelium) ni elementi ya kikemia yenye alama Bk na namba atomia 97. Ni metali nururifu iliyopangwa katika kundi la aktinidi kwenye mfumo radidia.

Berkeli haipatikani kiasili, ni elementi sintetiki. Ilitengenezwa mara ya kwanza kwenye mwaka 1949 na wanasayansi katika maabara ya Chuo Kikuu cha Kalifornia mjini Berkeley na kupokea jina la mji huo. Ilipatikana baada ya kufyatulia chembe alfa kwa atomi za Ameriki.

Berkeli ni haba sana, kiasi chote kilichotengenezwa tangu mwaka 1949 ni kama gramu 1. Haina matumizi nje ya utafiti wa kisayansi.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Tovuti nyingine[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Berkeli kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.