Beres Hammond

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Beres Hammond, Marekani 2013
Beres Hammond, Marekani 2013
Maelezo ya awali
Amezaliwa 28 Agosti 1955 (1955-08-28) (umri 68)
Annotto Bay, Jamaika
Aina ya muziki Reggae
Kazi yake Mwimbaji, mtunzi wa nyimbo, mtayarishaji wa rekodi
Miaka ya kazi 1972 – hadi
Studio VP Records
Tovuti vprecords.com/bereshammond

Beres Hammond (jina la kuzaliwa: Hugh Beresford Hammond; Annotto Bay, Saint Mary, Jamaica, 28 Agosti 1955) ni mwanamuziki wa mienendo ya reggae kutoka Jamaica ambaye hasa anajulikana katika mwenendo wa Lovers rock. Huku kazi yake katika fani ya muziki ikianza miaka ya 1970, alifikia mafanikio yake makuu mnamo miaka ya 1980.

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa wa tisa kati ya wana. Hammond alikua akiisikiza mikusanyiko ya soul na jazz iliyowekwa na babake; ikiwemo ile ya Sam Cooke na Otis Redding. Pia alishawishiwa zaidi na miziki ya humo nchini ya ska and rocksteady, hasa Alton Ellis.

Alianza kushiriki katika mashindano ya vipawa ya kwao kuanzia 1972 hadi 1973, ambayo yalimpelekea kurekodi wimbo wa kwanza kwa Ellis, "Wanderer". Mnamo 1975 alijiunga na bendi ya Zap Pow kama mwimbaji wa lead. Bendi hii ilikuwa na hit kutika kwa single yao "The System" iliyotayarishwa na lebo ya Aquarius Records . Hata hivyo pia alijishughulisha na muziki wa solo. Mnamo 1975 alitoa albamu yake ya kwanza ya Soul Reggae, in 1976. Ngoma zake za solo za "One Step Ahead" (1976) wimbo uliotayarishwa na Joe Gibbs "I'm in Love" (1978), zote zilikuwa hit nchini Jamaica. Aliachana na Zap Pow kuanza kazi yake kama mwanamuziki wa solo mnamo 1979. Alirekodi albamu mbili zaidi; Let's Make A Song mnamo 1980 na Red Light 1981. Aliunda kundi la Harmony la Tuesday's Children, ambalililizuru lakini halikurekodi.

Aliunda lebo yake ya kibinafsi ya Harmony Records mnamo 1985 kwa kutoka albamu yake ya Make a Song ambayo iliwahi kuwa na hit mbili katika chati kutokana na ushawishi wa mwenendo unaotokea wa dancehall; Groovy Little Thing" na "What One Dance Can Do". Ya pili ilitayrishwa na Willie Lindo na ilianza kumpaufanisi Hammond katika soko la kimataifa. Alipata hiti nyingine mnamo 1986 kutoka kwa wimbo wake "Settling Down". Aliacha umaarufu wake wa Jamaica na kuhamia New York mnamo 1987 baada ya kufungwa wakati wezi waliivamia nyumba yake katika uvamizi wa kinyumbani. Hapo alirekodi Have a Nice Weekend na single ya "How Can We Ease the Pain" iliyoshirikisha Maxi Priest.

Hammond alirejea Jamaica kurekodi Putting Up Resistance, ambayo ilikuwa ngumu zaidi kuliko miondoko mingine ya taratibu, chini ya Tapa Zukie, ambayo ilitoa hit kama "Putting Up Resistance" na "Strange." Alitia mkataba na lebo ya Penthouse Records mnamo 1990 na kurejea Jamaica rasmi huku akirekodi ngoma ya dancehall ya "Tempted to Touch" na mtayarishi Donovan Germain. Pengine huu ndio wimbo wake bora zaidi nchini Marekani na Ufalme wa Muunganona iliitilia msingi ngoma ya "Is This a Sign" na "Respect to You Baby" mnamo 1992 katika albamu ya Love Affair. Huku akihitajiwa na lebo nyingi zilizofahamika kama Elektra Records, Hammond alirekodi albamu tano zaidi mnamo miaka ya 1990 na pia albamu nyingi za mkusanyiko, huku akijiimarisha kama msanii mmojawapo bora zaidi katika mwenendo wa Lovers rock. Albamu yake ya kwanza ya mileniam mpya ilikuwa Music Is Life, iliyotolewa mnamo 2001 ambayo ilishirikisha uonekanaji wa Wyclef Jean. Toleo lake la 2004 la Love Has No Boundaries, lilishirikisha uonekanaji spesheli wa Buju Banton a Big Youth.

Alirejea Jamaica kutumbuiza katika sherehe za ufunguzi za Kombe la Dunia la Criketi la 2007.

Mnamo 2008 alitoa albamu nyingine "A moment in time" iliyoshirikisha single "I feel good". Ilitolewa mnamo 11 Novemba 2008 chini ya lebo ya VP Records.

Discografia[hariri | hariri chanzo]

Solo albamu[hariri | hariri chanzo]

  • Soul Reggae (1976), Water Lily
  • Just a Man (1979), VP [1]
  • Let's Make a Song (1981), Brotherhood Music Inc.
  • Red Light (1983), Heavybeat – recorded 1983
  • Beres Hammond (1985), VP [2]
  • Have A Nice Weekend (1988), VP [3]
  • A Love Affair (1992), Jet Star
  • Full Attention (1993), VP [4]
  • Sweetness (1993),VP [5]
  • In Control (1994), Elektra
  • Putting Up Resistance (1996), VP [6]
  • Lifetime Guarantee (1997), Greensleeves [7]
  • Love from a Distance (1997), VP [8]
  • A Day in the Life (1998), VP [9]
  • Music Is Life (2001), VP [10]
  • Love Has No Boundaries (2004), VP [11]
  • A Moment in Time (2008), VP – na DVD [12]
  • One Love, One Life (2012), VP [13]
  • Never Ending (2018), VP [14]

Albamu za Kolabo[hariri | hariri chanzo]

  • Expression (1995), Heartbeat – Beres Hammond & Derrick Lara [15]

Kompilesheni albamu[hariri | hariri chanzo]

  • Jet Star Reggae Max (1996), Jet Star
  • Beres Hammond: Collectors Series (1998), Penthouse
  • Beres Hammond and Friends (2001), Ejaness
  • Soul Reggae and More, Heavybeat
  • Can't Stop a Man: The Best of Beres Hammond (2003), VP [16]
  • Something Old Something New (2009), Penthouse

DVD[hariri | hariri chanzo]

  • Beres Hammond: Music is Life – Live From New York (2002), VP [17]

Tazama Pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Beres Hammond kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.