Benki ya Kimataifa kwa Afrika ya Magharibi (BIAO)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Benki ya Kimataifa kwa Afrika ya Magharibi (pia BIAO: kifupi cha Kifaransa kwa Banque Internationale pour l'Afrique Occidentale) ilikuwa benki ya Kifaransa iliyoanzishwa mnamo 1853 huko Dakar kama Benki ya Senegal ya Kifaransa.

Benki kwa koloni[hariri | hariri chanzo]

BIAO awali iliundwa kwa jina la "Banque du Senegal" mnamo 21 Desemba 1853. Benki hiyo ilipewa pia haki ya kutoa pesa rasmi kwa ajili ya koloni. Mwaka 1901 ilivunjwa rasmi na kuundwa upya kama "Banque de l’Afrique Occidentale" (BAO) yenye makao makuu mjini Paris. Iliruhusiwa kufanya kazi Senegal, Guinea ya Kifaransa, Cote d'Ivoire, Dahomey, Kongo pamoja na nchi nyingine upande wa magharibi wa Afrika zisizokuwa chini ya Ufaransa.

Benki ilifungua ofisi huko Conakry (Guinea) mwaka 1902, Porto-Novo (Dahomey) mnamo 1903, Grand-Bassam ( Cote d'Ivoire) 1905, Grand-Lahou 1908 na huko Assinie mwaka 1911 (Cote d’Ivoire). Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia benki iliendelea uufungua matawi Lomé (1922), Bamako (1925), Brazzaville (1925), Kaolack (1928) na Cotonou (1928).

Hadi mwaka 1955 BAO ilikuwa na kazi ya kutoa pesa kwa ajili ya koloni za Kifaransa katika Afrika. Tangu 1945 pesa hiyo ilikuwa tayari CFA-franc.

Mwaka 1955 serikali ya Ufaransa iliunda benki za pekee kwa Afrika ya Magharibiya ifaransa na kwa Afrika ya Ikweta ya Kifaransa, na BAO iliendelea kama benki binafsi ya kibiashara tu.

Wakati wa kufika kwa uhuru wa nchi za Kiafrika kwenye mwaka 1969 BAO ilikuwa na matawi 38 katika Afrika ilaendelea kuongeza moja huko Nigeria. Tawi nchini Guinea lilitaifishwa.

1965-1989: Benki ya Kimataifa kwa Afrika ya Magharibi (BIAO)[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 1965 wenye benki waliamua kushirikiana na benki ya First National City Bank ya New York; BAO ilifungwa na mali yake kuhamishwa kwenda Benki mpya ya Kimatifa kwa Afrika ya Magharibi (BIAO). Asilimia 51 za hisa zilikuwa mkononi mwa wenyeji Wafaransa, na asilimia 49 mkononi mwa Wamarekani.

Katika miaka ya 1970 matawi mbalimbali ya benki yalipaswa kufuata na siasa ya kiuchumi ya nchi zilizokuwepo. Utawala wa matawi ulihamia mkononi mwa watumishi Waafrika. Katika nchi mbalimbali matawi ya BIAO yalipata hadhi ya makampuni ya kitaifa chini ya benki mama.

Kwenye miaka ya 1980 benki ilipata matatizo ya kiuchumi na kufilisika. Mnamo 1991 utawala wa benki ilipitia mkononi mwa benki ya Kizambia; ilipofilisika mnamo 1995 BIAO kwa jumla ilikwisha. Matawi katika nchi kadhaa yaliendelea kama makampuni ya pekee na mengine yanaendelea kitumia jina la BIAO.

Jukumu la kiuchumi katika muundo wa kikoloni[hariri | hariri chanzo]

Wanahistoria kama Henri Brunschwig wameelezea umuhimu wa BOA katika uhamishaji wa Afrika Magharibi mwa Ufaransa katika mfumo wa uchumi wa Ufaransa.[1] Ilianzishwa mnamo 1901 ilikuja baada ya kupanuliwa kwa ushuru mdogo wa masomo, kulazimishwa sheria za kazi, na kupiga kura katika mali za wakoloni (haswa mawasiliano ya Dakar na Saint-Louis, Senegal). Uundaji na msaada wa serikali kwa BOA ilikuwa sehemu ya jaribio la kuingiza uwekezaji kwenye koloni za Ufaransa.

Mnamo 1880, karibu masilahi yote ya kiuchumi ya Ufaransa katika eneo hilo yalikuwa katika mfumo wa nyumba za biashara zinazoendeshwa na familia zilizo katika miji ya bandari ya Ufaransa kama Bordeaux na Marseille. Kuundwa kwa BOA kuliambatana na ujumuishaji wa nyumba hizi za biashara katika kampuni za pamoja za hisa, kumalizika kwa idhini rasmi ya serikali kwa nyumba hizi, na kuongezeka kwa ukiritimba wa ukweli wa warithi wao. [2].

Jukumu la kijamii katika muundo wa kikoloni[hariri | hariri chanzo]

Taasisi za kibenki, za umma na za kibinafsi, ziliwezesha wafanyabiashara wa kikoloni kuvuta zaidi uchumi wa Afrika Magharibi kuwa uchumi wenye pesa na kupanua uingizwaji wa kilimo cha jadi na mazao makubwa ya biashara ya kusafirishwa nje.[3] Hii ilikuwa dhahiri zaidi katika ukuaji mkubwa wa mashamba ya karanga.

Ofisi za BAO zilijengwa katika miji mikubwa yote ya Ufaransa Magharibi mwa Afrika, na majengo yao mazuri yakawa ishara ya nguvu ya kikoloni ya Ufaransa.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Henri Brunschwig: "Politique et Economie Dans l'Empire Francais d'Afrique Noire 1870-1914". The Journal of African History, Vol. 11, No. 3 (1970), pp. 401-417.
  2. Jean Suret-Canele. French Colonialism in Tropical Africa 1900-1945. Trans. Pica Press (1971), pp. 160-18
  3. Martin Thomas: The French Empire Between the Wars: Imperialism, Politics and Society. Manchester University Press (2005). ISBN 0-7190-6518-6

Kujisomea[hariri | hariri chanzo]

  • Jacques Alibert: De la vie coloniale au défi international: Banque du Sénégal, BAO, BIAO ; 130 ans de banque en Afrique - Chotard et Associés Éditeurs, 1983
  • Yves Ekoué Amaïzo: Naissance d’une banque de la zone franc, 1841-1901. La Banque du Sénégal- Paris, L’Harmattan, 2001.
  • Jean-Luc Aubert: Les billets de la banque de l'Afrique Occidentale. Chez l'auteur. Dépôt légal 1999