Benjamin Pavard

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pavard kwenye kombe la Dunia la 2018.

Benjamin Jacques Marcel Pavard (alizaliwa 28 Machi 1996) ni mchezaji wa soka wa Ufaransa ambaye anacheza kama beki wa klabu ya Bayern Munich na timu ya taifa ya Ufaransa. Yeye huchezeshwa hasa kama beki wa kati lakini pia anaweza kucheza kama beki wa kulia.

Alianza kazi yake na klabu ya Lille ya Ufaransa na baadae 2016 kuhamishiwa VfB Stuttgart ya Ujerumani. Mnamo Januari 2019 alikubali kuhamia Bayern Munich kwa mkataba wa miaka mitano hadi juni 2024.

Kimataifa aliisaidia nchi yake ya Ufaransa kushinda Kombe la Dunia la 2018, Yeye ndiye mchezaji aliyefunga goli bora zaidi katika michuano hiyo.


Football.svg Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Benjamin Pavard kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.