Nenda kwa yaliyomo

Bendera ya Kolombia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bendera ya Kolombia

Bendera ya Kolombia imepatikana tangu 26 Novemba 1861. Ina milia mitatu ya kulala ya njano, buluu na nyekundu. Mlia wa njano una nusu ya upana wa bendera, milia miwili mingine inachukua robo ya upana kila mmoja.

Rangi hizi tatu zilikuwa bendera ya Francisco de Miranda aliyekuwa mtangulizi wa Simon Bolivar kama mwanamapinduzi wa Amerika ya Kusini dhidi ya ukoloni wa Hispania. Bendera yake ilionekana mara ya kwanza katika Venezuela mwaka 1806.

Rangi hizi zinatumiwa na bendera za nchi tatu za Kolombia, Venezuela na Ekuador ambazo zote tatu zilikuwa sehemu ya jamhuri ya kwanza ya Kolombia ("Kolombia kubwa") hadi mwaka 1831.