Nenda kwa yaliyomo

Bella Angara

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Bellaflor Javier Angara-Castillo (alizaliwa 14 Septemba 1939), anajulikana zaidi kama Bella Angara, ni mwanachama wa zamani wa Baraza la Wawakilishi la Ufilipino (Philippine House of Representatives) akiwakilisha jimbo pekee la Aurora (lone district of Aurora).[1] Hapo awali, alihudumu kwa vipindi vitatu mfululizo kama gavana wa mkoa wa Aurora kuanzia mwaka 2004 hadi 2013, akiwa gavana wa tatu mwanamke katika mkoa huo. Kabla ya kuwa gavana, alihudumu pia kwa vipindi vitatu mfululizo kama mwakilishi wa jimbo hilo la Aurora kuanzia mwaka 1995 hadi 2004. Yeye ndiye mwanamke wa kwanza na wa pekee hadi sasa katika historia ya Bunge la Ufilipino (Philippine Congress) kuwa Kiongozi wa Sauti ya Wengi Bungeni (House majority floor leader).[2]

  1. ↑ Result of the May 13, 2013 Elections in the Province of Aurora Archived Desemba 28, 2013, at the Wayback Machine
  2. ↑ "Sons and Daughters: Municipality of Baler (Aurora)". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-08-10. Iliwekwa mnamo 2026-05-20.
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Bella Angara kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.