Nenda kwa yaliyomo

Bekzod Abdurakhmonov

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bekzod Abdurakhmonov upande wa kulia dhidi ya Jabrayil Hasanov kwenye Olimpiki ya mwaka 2016
Bekzod Abdurakhmonov upande wa kulia dhidi ya Jabrayil Hasanov kwenye Olimpiki ya mwaka 2016

Bekzod Makhamadzhonovich Abdurakhmonov (kwa Kirusi: Бекзод Махамаджонович Абдурахмонов; amezaliwa Machi 15, 1990) ni mpiganaji wa mieleka wa Uzbekistani.

Alishinda medali ya dhahabu katika Michezo ya Asia ya 2014 katika  mchezo wa mieleka wa wanaume wenye uzito  wa kilo 70.[1] Katika michezo ya Olimpiki ya 2016 alimshinda mshindi wa dhahabu wa zamani kutokea Marekani Jordan Burroughs, lakini akashindwa katika mechi ya medali ya shaba na Jabrayil Hasanov wa Azerbaijan. Alishinda moja ya medali za shaba katika michezo ya Olimpiki majira ya joto ya 2020 kwa wanaume wenye uzito wa kilo 74  huko Tokyo, Japani.[2][3]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-08-30. Iliwekwa mnamo 2021-11-29.
  2. IOC (2018-04-23). "Tokyo 2020 Summer Olympics - Athletes, Medals & Results". Olympics.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-11-29.
  3. "Bekzod ABDURAKHMONOV". Olympics.com. Iliwekwa mnamo 2021-11-29.