Nenda kwa yaliyomo

Becquerel

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Becquerel (alama: Bq) ni kizio cha upimaji wa unururifu, kimoja cha vipimo vya SI.

Becquerel imefafanuliwa kama kiwango cha unururifu kinachotokana kwa mbunguo wa kiini cha atomu kimoja kwa sekunde moja.

Kiwango hicho ni kidogo sana kwa vipimo vyote vinavyohusu afya ya binadamu na hivyo kwa kawaida vigawe vya Bq hutumiwa. Vigawe vya kawaida ni:

  • kBq (kilobecquerel, 103 Bq)
  • MBq (megabecquerel, 106 Bq, sawa na rutherford 1)
  • GBq (gigabecquerel, 109 Bq)
  • TBq (terabecquerel, 1012 Bq)
  • PBq (petabecquerel, 1015 Bq)
  • EBq (exabecquerel, 1018 Bq)
  • YBq (yottabecquerel, 1024 Bq)

Becquerel ilichukua nafasi ya vipimo visivyo vya SI kama curie na rutherford.

Jina lilichaguliwa kwa heshima ya mwanafizikia Mfaransa Antoine Henri Becquerel aliyepokea Tuzo ya Nobel ya Fizikia kwenye mwaka 1903 pamoja na Pierre Curie na Marie Curie.

Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Becquerel kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.