Becky Umeh
| Becky Umeh | |
| Amezaliwa | Becky UzoAmaka Umeh Anambra State, Nigeria |
|---|---|
Umeh alizaliwa katika Jimbo la Anambra, Nigeria, lakini alikulia Lagos kuanzia akiwa na umri wa miaka mitano. Mnamo mwaka 1992, alipata umaarufu wa kitaifa kama mwigizaji katika tamthilia ya watoto ya Shirika la Televisheni la Nigeria (Nigerian Television Authority) iitwayo Tales by Moonlight. Pia alishiriki katika filamu huru kama Jezebel, Twist of Fate, Living Ghost, na Amazon, miongoni mwa nyingine.
Kuanzia 1994 hadi 1998, Umeh alisomea ngoma za jadi na za kisasa za Kiafrika kwa ufadhili kamili katika Ivory Dance Academy, iliyoanzishwa na Steve James, mjumbe wa National Troupe of Nigeria. Akiwa masomoni, alifanya ziara na kundi la shule hiyo liitwalo Ivory Ambassadors, na akafanya utafiti wa nyanjani kuhusu ngoma za jadi katika vijiji vya Nigeria.
Baada ya kuhitimu masomo yake, Umeh alihudumu kama Mkurugenzi wa Ngoma wa Ivory Dance Troupe kwa kipindi cha miaka mitano, akiongoza na kutayarisha maonesho kwa kampuni kama Guinness, Mobile, Chevron, Seven-Up Bottling Company, na nyinginezo. Baada ya ziara fupi nchini Ghana, alisafiri kwenda Paris wakati wa Kombe la Dunia la FIFA la mwaka 1998 akiwa pamoja na timu ya taifa ya soka ya Nigeria. Becky Umeh alianza rasmi taaluma yake ya uimbaji na akaanzisha bendi yake, na kwa pamoja wakatayarisha albamu iliyoitwa Aiye.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]| Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Becky Umeh kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |