Beatrice Aboyade
| Beatrice Olabimpe Aboyade | |
| Faili:Beatrice Aboyade.png | |
| tarehe ya kuzaliwa | 24 Agosti 1935 Ijebu Ode, Ogun State |
|---|---|
| tarehe ya kufa | 3 Machi 2023 (umri 87) |
| jina ya kuzaliwa | Beatrice Olabimpe |
| ndoa | Professor Ojetunji Aboyade (deceased) |
| watoto | 4 |
| mhitimu wa | University of Ibadan University of Michigan |
| taaluma | Librarian |
Beatrice Aboyade (24 Agosti 1935 - 3 Machi 2023) alikuwa mkutubi wa kutoka nchi ya Nigeria na pia alikua ni profesa wa Mafunzo ya Maktaba kwenye Chuo Kikuu cha Ibadan. Alijulikana kama mpainia kwenye Ukutubi nchini Nigeria na World Encyclopedia of Library and Information Services. Aboyade likua mfanyakazi kwenye Chuo Kikuu cha Ibadan na Maktaba za Chuo Kikuu cha Ile-Ife . [1] [2] [3]
Maisha ya awali na elimu
[hariri | hariri chanzo]Aboyade alisomea masomo yake ya msingi kwenye Shule ya Msingi ya Christ's Church, Porogun, Ijebu Ode . Aliisonga mbele na elimu yake ya sekondari katika Chuo cha Queen's, Lagos, kwenye miaka katikati ya 1948 na 1951. Kipindi cha 1952 na 1953, alihitimisha shule yake ya sekondari kwenye Chuo cha Queen's, Ede. Alipata elimu ya shahada yake ya kwanza ya Kiingereza kutoka Chuo Kikuu cha Ibadan mwaka wa 1960, baada ya hapo akaendelea na shahada zaidi akiwemo Chuo Kikuu cha Michigan mwaka wa 1964. Kwenye mwaka 1970, alihitimisha udaktari wake kwenye Chuo Kikuu cha Ibadan.
Alifunga ndoa na na Profesa Ojetunji Aboyade, profesa wa uchumi, kuanzia mwaka 1961 hadi kifo chake baba huyo kwenye mwaka wa 1994. [4]
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Aboyade hakushika nafasi ya mkutubi mara moja bali alitumia muda mfupi kakwenye tika Shirika la Utangazaji la Nigeria kabla ya kujiunga na maktaba ya Chuo Kikuu cha Ibadan kama mkutubi msaidizi mnamo 1962. Kisha baada ya muda mfupi alipata nafasi mpya kama mkusanyaji mkuu wa orodha kwenye Chuo Kikuu cha Ife mwaka wa 1965. Miaka mitatu mbeleni alirudi Chuo Kikuu cha Ibadan kusimamia Huduma zao za Wasomaji. Mwaka wa 1972 alikua akitoa mafundisho mahali alipokuwa mhadhiri wa chuo kikuu katika idara ya sayansi ya maktaba. [5]
Kwenye mwaka wa 1978, alipanda cheo hadi cheo kutoka mhadhiri mkuu akahaguliwa kuwa profesa wa masomo ya maktaba kwenye Chuo Kikuu cha Ibadan, [6] na alihudumu kama mkuu wa idara ya Maktaba, Kumbukumbu na Mafunzo ya Habari katika chuo kikuu. [7] Pia alisimamia Mfumo wa Taarifa za Maendeleo Vijijini (RUDIS), ambao uliongeza upatikanaji wa taarifa na maarifa kwa watu wa vijijini bara la Afrika . [8] Kazi yake na RUDIS iliweka wazi kwamba maktaba za vijijini za Nigeria zilitimiza mahitaji ya utendaji kazi. Vitabu vya maktaba vilitumika kuonyesha jinsi ya kuweka vizuri zaidi huduma za umma kama vile barabara, umeme, fedha na maji ya bomba. Wasomaji wange elimika juu ya fursa za ajira zisizo za eneo hilo tu au nchini humo tu pamoja na taarifa kuhusu mbolea na fursa za biashara. [6]
Kifo
[hariri | hariri chanzo]Aboyade alifariki tarehe 3 Machi 2023, akiwa makamu wa miaka 87.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Wedgeworth, Robert (1993). World Encyclopedia of Library and Information Services. Chicago: American Library Association. ku. 1. ISBN 9780838906095.
- ↑ Nigerian Women Annual: Who's Who. Benin City: Gito & Associates. 1990. uk. 15. ISSN 0795-7807.
- ↑ "Beatrice Aboyade". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 19 Mei 2021. Iliwekwa mnamo 19 Mei 2021.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "ABOYADE, Prof. (Mrs.) Beatrice Olabimpe". Biographical Legacy and Research Foundation. 19 Julai 2016. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 1 Julai 2019. Iliwekwa mnamo 9 Juni 2018.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Robert, Wedgeworth (1993). World Encyclopedia of Library and Information Services (tol. la 3). America: America Library Association. uk. 1. ISBN 0838906095. Iliwekwa mnamo 8 Februari 2019.
{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - 1 2 Robert, Wedgeworth (1993). World Encyclopedia of Library and Information Services (tol. la 3). America: America Library Association. uk. 1. ISBN 0838906095. Iliwekwa mnamo 8 Februari 2019.
{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)Robert, Wedgeworth (1993). World Encyclopedia of Library and Information Services (3 ed.). America: America Library Association. p. 1. ISBN 0838906095. Retrieved 8 February 2019. - ↑ "ABOYADE, Prof. (Mrs.) Beatrice Olabimpe". Biographical Legacy and Research Foundation. 19 Julai 2016. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 1 Julai 2019. Iliwekwa mnamo 9 Juni 2018.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)"ABOYADE, Prof. (Mrs.) Beatrice Olabimpe". Biographical Legacy and Research Foundation. 19 July 2016. Archived from the original on 1 July 2019. Retrieved 9 June 2018. - ↑ Wedgeworth, Robert (1993). World Encyclopedia of Library and Information Services. Chicago: American Library Association. ku. 1. ISBN 9780838906095.Wedgeworth, Robert (1993). World Encyclopedia of Library and Information Services. Chicago: American Library Association. pp. 1. ISBN 9780838906095.