Nenda kwa yaliyomo

Beastie Boys

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Beastie Boys
A group of three men on a stairwell in front of a light background
Beastie Boys mnamo 2009. Kush-kulia: Ad-Rock, MCA, na Mike D.
Taarifa za awali
ChimbukoNew York City, U.S.
Aina ya muziki
Miaka ya kazi1979–2012
Studio
Wavutibeastieboys.com

Beastie Boys ilikuwa kundi la muziki wa hip hop na rap rock kutoka New York City, Marekani, lililoanzishwa mwaka 1979.[1] Kundi hili lilihusisha wanachama watatu: Adam "Ad-Rock" Horovitz (mwimbaji, gitaa), Adam "MCA" Yauch (mwimbaji, besi), na Michael "Mike D" Diamond (mwimbaji, ngoma).

Beastie Boys lilianza kama sehemu ya bendi ya hardcore punk iliyoitwa Young Aborigines, ambayo iliundwa mwaka 1979 ikiwa na Diamond (ngoma), Jeremy Shatan (gitaa la besi), John Berry (gitaa), na Kate Schellenbach (tumba).[2] Shatan alipohamia New York mwaka 1981, Yauch alichukua nafasi yake kwenye besi, na bendi ikabadili jina kuwa Beastie Boys. Berry aliondoka muda mfupi baadaye na nafasi yake ikachukuliwa na Horovitz.

Baada ya kupata umaarufu wa ndani kupitia wimbo wa ucheshi wa hip hop "Cooky Puss" mnamo 1983, Beastie Boys walijikita kikamilifu katika muziki wa hip hop, na Schellenbach akaondoka kundini. Mwaka 1985, walijiunga na Madonna kwenye ziara yake, na mwaka mmoja baadaye wakatoa albamu yao ya kwanza, Licensed to Ill (1986), ambayo ilikuwa albamu ya kwanza ya rap kufika kileleni kwenye chati ya Billboard 200.[3] Albamu yao ya pili, Paul's Boutique (1989), ambayo ilitegemea sana sampuli ya nyimbo nyingine, haikufanya vizuri kibiashara mwanzoni lakini baadaye ikasifiwa na wakosoaji. Albamu zilizofuata kama Check Your Head (1992), Ill Communication (1994), Hello Nasty (1998), To the 5 Boroughs (2004), The Mix-Up (2007), na Hot Sauce Committee Part Two (2011) zilipokelewa vizuri na mashabiki.

Beastie Boys wameuza zaidi ya nakala milioni 20 nchini Marekani na kati ya 1986 na 2004 walitoa albamu saba zilizopata vyeti vya platinamu.[4] Ni kundi la rap lililouza zaidi tangu Billboard ilipoanza kurekodi mauzo mwaka 1991.[5] Mwaka 2012, walikuwa kundi la tatu la rap kuingizwa katika Rock and Roll Hall of Fame. Katika mwaka huo huo, Yauch alifariki kutokana na saratani na kundi likavunjika.[6] Wanachama waliobaki waliendelea kutoa kazi za kumbukumbu, ikiwa ni pamoja na kitabu, makala ya filamu, na albamu ya mchanganyiko wa nyimbo zao bora. Kundi hili ni sehemu ya Kizazi cha dhahabu cha hip hop.

Diskografia

[hariri | hariri chanzo]

Albamu za Studio

Filmografia

[hariri | hariri chanzo]
  • Beastie (1982)
  • Krush Groove (1985)
  • Tougher Than Leather (film)|Tougher Than Leather (1988)
  • Futurama kisa cha "Hell Is Other Robots" (1999)
  • Awesome; I Fuckin' Shot That! (2006)
  • Fight for Your Right Revisited (2011)
  • Beastie Boys Story (2020)
  • Light, Alan (2006). The Skills to Pay the Bills: The Story of the Beastie Boys. Three Rivers Press. ISBN 978-0-6096-0478-6.
  1. Erlwine, Stephen. "Beastie Boys: Biography". AllMusic. RhythmOne Group. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Oktoba 19, 2018. Iliwekwa mnamo 6 Novemba 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Exclaim! Canada's Music Authority". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-07-14. Iliwekwa mnamo 2008-08-24.
  3. Burkett, Jacob (Novemba 16, 2016). "8 Things You Didn't Know About The Beastie Boys' Licensed To Ill". Moshcam. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Juni 4, 2020. Iliwekwa mnamo Aprili 2, 2020.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Obituary: Adam 'MCA' Yauch". BBC News. Mei 4, 2012. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Mei 8, 2012. Iliwekwa mnamo Mei 9, 2012.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. Caulfield, Keith (Mei 4, 2012). "Beastie Boys Blazed Billboard Chart History". Billboard. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Februari 4, 2013. Iliwekwa mnamo Mei 4, 2012.{{cite magazine}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. Gordon, Jeremy (Juni 2, 2014). "Mike D Says Beastie Boys Won't Be Making Any More Music". Pitchfork. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Juni 4, 2014. Iliwekwa mnamo Juni 2, 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]