Bazedoxifene na mchanganyiko wa estrojeni
| Data ya kikliniki | |
|---|---|
| Majina ya kibiashara | Duavee, Duavive |
| AHFS/Drugs.com | Monograph |
| MedlinePlus | a614004 |
| Taarifa za leseni | US Daily Med:link |
| Kategoria ya ujauzito | D(AU) X(US) |
| Hali ya kisheria | ℞-only (US) ℞ Prescription only |
| Njia mbalimbali za matumizi | Kwa mdomo |
| Vitambulisho | |
| Nambari ya ATC | ? |
| Data ya kikemikali | |
| Fomyula | ? |
Bazedoxifene na mchanganyiko wa estrojeni, zinazouzwa kwa jina la chapa Duavee na Duavive, ni dawa mchanganyiko inayotumika kutibu dalili za kukoma hedhi na mifupa ambayo imepoteza uimara wake (osteoporosis) baada ya kukoma hedhi.[1] Dawa hii inamezwa kwa mdomo[2] na inapaswa kutumika kwa muda mfupi.[2]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na mkazo wa misuli, kichefuchefu, kuhara, kiungulia, kizunguzungu, na maumivu.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha kuganda kwa damu, kiharusi, na saratani ya ukuta wa ndani wa tumbo la uzazi (endometrial cancer).[1] Dawa hii haipaswi kutumika wakati wa ujauzito.[2] Ina bazedoxifene, kirekebishaji maalumu cha vipokezi vya homoni ya estrojeni, na mchanganyiko wa homoni za estrojeni.[3]
Mchanganyiko huo uliidhinishwa kwa matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2013 na Ulaya mwaka wa 2014.[1][4] Nchini Marekani, dawa ya mwezi mmoja iligharimu takriban dola za Marekani 180 kufikia mwaka wa 2022.[5]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- 1 2 3 4 "Selective Estrogen Receptor Modulators". LiverTox: Clinical and Research Information on Drug-Induced Liver Injury. National Institute of Diabetes and Digestive and Kidney Diseases. 2012. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 11 Januari 2022. Iliwekwa mnamo 8 Januari 2022.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - 1 2 3 "DailyMed - DUAVEE- conjugated estrogens/bazedoxifene tablet, film coated". dailymed.nlm.nih.gov. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 10 Mei 2021. Iliwekwa mnamo 8 Januari 2022.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Bazedoxifene Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 19 Aprili 2021. Iliwekwa mnamo 8 Januari 2022.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Duavive EPAR". European Medicines Agency (EMA). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-06-10. Iliwekwa mnamo 2020-06-10.
- ↑ "Conjugated Estrogens and Bazedoxifene Prices, Coupons & Savings Tips - GoodRx". GoodRx. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 16 Aprili 2016. Iliwekwa mnamo 8 Januari 2022.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)