Bayburt

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 16:59, 9 Machi 2013 na Addbot (majadiliano | michango) (Bot: Migrating 33 interwiki links, now provided by Wikidata on d:q211828 (translate me))
Picha mji wa Bayburt

Bayburt (Kiarmenia: Բաբերդ, Baberd) ni mji mkuu wa Mkoa wa Bayburt katika nchi ya Uturuki.

Bayburt ulikuwa mji muhimu kabisa wakati wa zama za Barabara ya Hariri na pia mji ulipatwa kutembelewa na mpelelezi Marco Polo na msafiri wa Kituruki Bw. Evliya Celebi. Huko pia kuna mabaki ya mangome ya Ufalme wa Byzantini ambayo hadi leo hii bado yapo.

Kuna misikiti kibao ya kuvutia, kuna mamawe kadhaa ya kituruki ikiwa sambamba kabisa na Miji ya Chini ya Catalcesme na pamoja na Mapolomoko ya Maji ya Sirakayalar.

Historia

Tarehe kamili ya kuanzishwa kwa mji huu wa Bayburt bado haijulikani. Ingawa, kuwa inakisiwa kwamba utakuwa umeanzishwa kunako mwaka 100 KK. Mji wa Bayburt unafahamika zaidi kwa kuwa ulishawahi kumilikiwa na Dola la Roma na baada ya mgawiwo wa miji ukaja kuwa moja kati ya miji ya Roma ya Mashariki.

Wakati wa zama za Byzantini, Bayburt ulikuwa moja kati ya majimbo ya kujitawa ya Byzantine na uliitwa Heldia ukiwa kama wa 4 katika migawiwo yao ya miji saba iliyotengwa.

Mji pia unajulikana kwa ngome iliyorekebishwa na mfalme wa Byzantine maarufu kama Mfalme Justinia I, lakini baadaye mji ulipolwa na Waarabu. Waturuki walishikiria madaraka ya mji huo kwa mara ya kwanza mnamo 1054, na baada ya miaka 200 baadaye mji ukawa unashikiriwa na madola tofauti-tofauti.

Viungo vya nje