Batamiti
Mandhari
| Batamiti | ||||||||||||||
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
| Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
| Ngazi za chini | ||||||||||||||
|
Spishi 8:
|
Mabatamiti au Dendrocygninae ni nusufamilia ya familia ya Anatidae yenye jenasi moja tu, Dendrocygna. Waainishaji wengine wanawaweka ndani ya familia yao wenyewe Dendrocygnidae au ndani ya kabila Dendrocygnini ya familia ndogo Anserinae. Leo kuna spishi nane za mabatamiti na visukuku vya spishi ingine vimefunuliwa kisiwani kwa Aitutaki, Visiwa vya Cook. Wanaitwa mabatamiti kwa sababu hujenga matago yao pengine ndani ya miti. Lakini kwa Kiingereza wanaitwa “whistling ducks” sikuhizi kwa sababu ya sauti yao kama mluzi. Mabata hawa wanatokea popote kwa kanda za tropiki na nusutropiki. Wana miguu mirefu na shingo refu na wanapenda kuwa pamoja. Makundi makubwa ya ndege hawa huonekana maziwani.
Spishi za Afrika
[hariri | hariri chanzo]- Dendrocygna bicolor, Batamiti Kahawia (Fulvous Whistling Duck)
- Dendrocygna viduata, Batamiti Uso-mweupe (White-faced Whistling Duck)
Spishi za mabara mengine
[hariri | hariri chanzo]- Dendrocygna arborea (West Indian Whistling Duck)
- Dendrocygna arcuata (Wandering Whistling Duck)
- Dendrocygna autumnalis (Black-bellied Whistling Duck)
- Dendrocygna eytoni (Plumed Whistling Duck)
- Dendrocygna guttata (Spotted Whistling Duck)
- Dendrocygna javanica (Lesser Whistling Duck)
Picha
[hariri | hariri chanzo]- Batamiti kahawia
- Batamiti uso-mweupe
- West Indian whistling duck
- Wandering whistling duck
- Black-bellied whistling duck
- Plumed whistling duck
- Spotted whistling duck
- Lesser whistling duck