Bata, Guinea ya Ikweta
Bata | |
Kosa la Lua katika Module:Location_map kwenye mstari wa 522: Unable to find the specified location map definition: "Module:Location map/data/Equatorial Guinea" does not exist. Mahali pa Bata |
|
Majiranukta: 01°51′54″N 09°46′12″E / 1.86500°N 9.77000°E | |
Nchi | ![]() |
---|---|
Mkoa | Litoral |
Mwinuko | 5 m (16.4 ft) |
Idadi ya wakazi (2012) | |
- Wakazi kwa ujumla | 250,770 |
Jina la watu | Batense (mmoja) Batenses (wengi) |
Kodi ya simu | 08 |
Tabianchi | Am |
Bata ni mji mkubwa wa jamhuri ya Guinea ya Ikweta, katika wilaya ya Litoral. Ni mji wa bandari na makao makuu ya wilaya hiyo na pia ya kanda ya Rio Muni ambayo ni sehemu ya kibara ya nchi. Mwaka 2015 idadi ya watu ilikadiriwa kuwa 290,000 na hivyo ni mji mkubwa wa nchi hiyo.
Uko kwenye pwani a Bahari ya Atlantiki ya eneo la bara la nchi. Bata ni kitovu cha usafiri na bandari, ambapo feri husafiri hadi mji mkuu Malabo na jiji la Douala nchini Kamerun, wakati ndege zinaweza kutua katika Uwanja wa Ndege wa Bata.
Bandari ya Bata ni kati ya bandari zenye kina kirefu zaidi katika Afrika ya Magharibi. Hata hivyo, Bata haina beseni la asili na gati lilijengwa ili kusaidia uhamisho wa shehena za meli. Bidhaa kuu zinazouzwa nje ni mbao na kahawa. [1] Bandari hiyo ilipanuliwa kwa sehemu na mikopo ya ushirikiano wa China, na uwezo wake ni tani milioni 6,5 na kontena za TEU 300,000 kila mwaka. [2]
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Encyclopædia Britannica, Retrieved on June 18, 2008
- ↑ BRI and International Cooperation in Industrial Capacity: Industrial Layout Study, Xu Shaoshi Routledge, 14 June 2020
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Bata, Guinea ya Ikweta kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |