Nenda kwa yaliyomo

Barbara Ehrenreich

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Barbara Ehrenreich

Barbara Ehrenreich (26 Agosti 19411 Septemba 2022) alikuwa mwandishi na mwanaharakati wa kisiasa kutoka Marekani. Wakati wa miaka ya 1980 na mwanzoni mwa miaka ya 1990, alikuwa mtu mashuhuri katika chama chake cha Democratic Socialists of America (DSA). Alikuwa mwandishi maarufu wa makala za magazeti na insha, alifanikiwa kuandika vitabu 21 na kushinda tuzo kadhaa. Ehrenreich alipata umaarufu mkubwa kupitia kitabu chake cha mwaka 2001, Nickel and Dimed: On (Not) Getting By in America, ambacho ni kumbukumbu ya miezi mitatu aliyojaribu kuishi kwa kufanya kazi za mshahara wa chini. Alitunukiwa Tuzo ya Fasihi ya Lannan na Tuzo ya Erasmus kwa mchango wake wa kipekee katika fasihi na jamii..[1][2]

Barbara Ehrenreich alizaliwa Butte, Montana, mwaka 1941. Alikulia katika familia yenye misimamo ya kisiasa ya mrengo wa kushoto na baadaye alijitambulisha kama asiyemwamini Mungu, ingawa alipata uzoefu wa kiroho wa aina ya animism (imani ya kitamaduni kwamba kila kitu kilicho hai na kisicho hai, kama vile wanyama, miti, mawe, mito au milima, kina roho au nguvu ya kiroho inayokiendesha au kukipa uhai). Alisomea fizikia na kemia katika Chuo cha Reed, Baadaye alipata Shahada ya Uzamivu (Ph.D.) katika taaluma ya kinga ya mwili kutoka Chuo Kikuu cha Rockefeller. Tukio la kumzaa binti yake mwaka 1970 lilimhamasisha kuwa mwanafeministi. Badala ya kufuata taaluma ya kisayansi, alijikita katika utafiti, harakati na uandishi kuhusu afya ya wanawake, ujamaa wa kifeministi na masuala ya kijamii.

  1. Ehrenreich, Barbara. "About Barbara". barbaraehrenreich.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Juni 23, 2011. Iliwekwa mnamo Mei 8, 2011.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Papers of Barbara Ehrenreich, 1922–2007 (inclusive), 1963–2007 (bulk): A Finding Aid". Arthur and Elizabeth Schlesinger Library on the History of Women in America, Radcliffe Institute for Advanced Study, Harvard University. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Desemba 16, 2011. Iliwekwa mnamo Mei 8, 2011.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Barbara Ehrenreich kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Viungo Vya Nje

[hariri | hariri chanzo]