Barakoa katika janga la corona 2019-20

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mtu aliye vaa Barakoa katika janga la corona 2019-20

Uvaliaji wa barakoa katika janga la corona miaka 2019-2020 umepata mapendekezo mbalimbali kutoka idara mbalimbali za afya pamoja na serikali. Mada hii imekuwa chanzo cha mjadala ambao umeifanya serikali pamoja na idara za afya kutokubaliana katika itifaki za dunia kuhusu uvaliaji wa barakoa.

Matokeo ya kufikia[hariri | hariri chanzo]

Zifuatazo ni baadhi ya sababu zilizotolewa na maafisa wa afya wa Uchina wakati wa janga la corona 2019-20 kuhusu umma kuvalia barakoa:[1]

 1. Kusambaa bila dalili (maambukizi kutoka wale ambao hawaonyeshi dalili zozote). Watu wengi wanaweza kuambukizwa bila dalili ama na dalili yenye makali chache.
 2. Kutowezekana kwa watu kukaa mbali na wenzao katika maeneo ya umma wakati wote.
 3. Kukatishwa tamaa juu ya kutofaidika kiuchumi. Iwapo walioambukizwa na ugonjwa huu, wanauwezekano wa kukatishwa tamaa wakifanya hivyo. Kuna uwezekano kwa yule aliyeambukizwa asiweze kupata jambo lolote zuri, ila tu atagharamia fedha kama zile za kununua vitu.

Stephen Griffin ambaye ni mwanasayansi wa virusi katika chou kikuu cha Leeds anasema, “Kuvalia barakoa inaweza zuia watu kushika nyuso zao, jambo ambalo ni sababu moja kuu ya watu kuambukizwa bila kuzingatia elimusiha ya mikono."[2]

Aina za barakoa[hariri | hariri chanzo]

Barakoa ya nguo ni barakoa iliyotengenezwa na nguo ya pamba, inayovaliwa katika pua na mdomo. Tofauti na barakoa ya upasuliaji na ile mashine ya kusaidi kupumua, barakoa ya aina hii haizuiliwi. Sasa hivi kuna utafiti mchache kuhusu ufanisi kama mojawapo ya kinga kutokana na ugonjwa unaoweza kusambaa kwa urahisi au kutoka machafuko ya hewa.

Barakoa ya upasuliaji ni ya kupwaya, na kifaa cha kuondolewa inayotengeneza kizuizi kati ya pua na mdomo ya anayeivalia na visababishi vyenye uwezo wa kuchafua mazingira. Barakoa hii ni ya kusaidia katika kuzuia matone kubwa ya chochote kinachoweza kuwa na virusi na vijududu kama havijavaliwa vizuri na kwa njia hii, barakoa hii inazuia vitu hivyo kufika kwenye mdomo na mapua ya aliyevaa. Barakoa hii ya upasuliaji yaweza saidia kuzuia mfichuo wa mate ya anayeivalia kwa wengine.[3] Pia, barakoa hii haijaundwa kuchuja au kuzuia chembe ndogo za hewa zinazoweza kuambukizwa kwa kukohoa, kupiga chafya ama njia kadhaa za matibabu. Barakoa za upasuliaji huwa hazitoi usalama kamili dhidi ya uchafu wowote kwa sababu ya jinsi inavyokosa kushikilia vyema eneo ya pua na mdomo inayofaa kushikilia. Barakoa hii imetengenezwa kutoka vitambaa ambavyo havijafumwa.[4][5]

Barakoa aina ya N95 ni barakoa inayohaswa chuja hewa inayoafikiana na daraja la taasisi la kitaifa ya kazi, usalama na afya ya nchi ya Marekani. Barakoa hii inachuja angalau asilimia tisini na tisa ya chembe inayosambaa hewani.[6]

Mapendekezo Ya Mashirika ya Afya[hariri | hariri chanzo]

Mashirika ya afya yamependekeza ya kuwa watu wafunike midomo na mapua yao kwa kutumia kiwiko iliyopinda ama karatasi shashi kila wakati wanapokohoa ama kupiga chafya. Na pindi tu wanapomaliza kuitumia karatasi shashi, wanafa kuitupa.[7][8]

Barakoa za upasuliaji zinapendekezwa kwa wale ambao wameambukizwa kwa sababu kuvalia barakoa hii inazuia umbali wa matone yanayotoka wakati mtu anaongea,[9][10][11] kupiga chafya ama kukohoa.[12]

Mapendekezo ya Shirika la Afya Duniani[hariri | hariri chanzo]

Shirika la Afya Duniani linashauri umma katika muktadha wa COVID-19 iliyopitisha kutumia barakoa ila tu katika hali zifuatazo[13]:

 • Iwapo ukomzima kiafya, unahitajika kuvalia barakoa kama unamlinda mtu yeyote anayetuhumiwa na 2019-nCoV
 • Vaa barakoa ikiwa unakohoa ama kupiga chafya.
 • Barakoa inafaa kama tu inatumiwa wakati mtu anaosha mikono kutumia maji na sabuni
 • Ikiwa unatumia barakoa, unafaa kujua jinsi ya kuitumia na pia jinsi ya kuiondoa vyema

Matumizi ya barakoa na sera zilizowekwa barani Afrika[hariri | hariri chanzo]

 • Benin: Kutoka Aprili 8, serikali ya Benin ilianza kutekeleza uvaliaji wa barakoa ni lazima ili kusimamisha virusi vya Corona[14]
 • Cameroon: Meya wa mji wa Cameroon alitangaza ya kuwa kuvalia barakoa itakuwa lazima ilikupunguza maambukizi ya virusi hivi vya corona[15]
 • Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo: Uvaliaji wa barakoa sasa ni lazima katika jiji lote kuu.[16]
 • Ethiopia: Baraza la mawaziri lilikubali kanuni inayopiga marufuku kusalimiana kwa mikono na inatoa masharti ya kuvalia barakoa katika maeneo ya umma.[17]
 • Guinea: Alpha Conde ambaye ni Rais wa nchi hii aliamua kuweka uvaliaji wa barakoa kuwa lazima[18]
 • Kenya: Uvaliaji wa barakoa ni lazima. Serikali imeweka wakenya kufuata masharti ya kuzingatia umbali wa nafasi baina ya watu, swala ambalo limethihirika kuwa njia dhabiti ya kuzuia watu kuambukizwa.[19]
 • Liberia: Kutoka Aprili 21, imekuwa ni lazima kuvalia barakoa katika umma[20]
 • Morocco: Kuvalia barakoa ni lazima[21]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. “Mbona Wachina ambao wako wazima wanavalia barakoa nje ya nyumba?” NHC.gov.cn
 2. “Jinsi ya kuzuia kushika uso wako kw asana” Habari za BBC Machi 18 2020
 3. Ruka hadi ab “N95 Vipumzi na barakoa za upasuliaji” Utawala wa Marekani, Chakula na Dawa Machi 11 2020. Ilipatwa Machi 28 2020. Makala haya yanahusisha ujumbe kutoka chanzo hiki, ambacho ni cha umma.
 4. “Sii barakoa za kutosha zinazotengenezwa Marekani ili kukabiliana na virusi vya Corona” NPR.org. 5 Machi 2020. Ilipatwa Aprili 10 2020
 5. “Watengenezaji wachina wa barakoa wanatumia mianya ili kuharakisha udhibiti kibali.” Wakati wa Fedha 1 Aprili 2020. Ilipatwa Aprili 10 2020
 6. Kipumzi, Chanzo kinachoaminika: Mchaguo, Maswali na majibu yanayoulizwa. Shirika la kitaifa la usalama na afya. Machi 12 2020. Ilipatwa Machi 28 2020.
 7. “Ushauri kwa umma” Shirirka la afya duniani. Ilipatwa Februari 8 2020
 8. Nyumbani. “Riwaya ya virusi vya corona.” HPSC, Utetezi na uangalizi wa afya ya Ireland. Ilipatwa Februari 27 2020.
 9. Magonjwa sahihi ya kupumua yanayohusiana na riwaya ya ajenti ya kuambukizwa.” Serikali ya Hong Kong. Ilipatwa Februari 2020
 10. Taarifa kuhusu virusi ya corona Wuhan (2019-nCoV) hali ya kienyeji” MoH.gov.sg. Wizara ya afya ya Singapore. Ilipatwa Februari 1 2020
 11. Ruka hadi a b c Ushauri kuhusu kutumia barakoa katika jamii, wakati wa utunzaji wa nyumbani katika muktadha wa riwaya virusi wa corona (2019-nCoV). Shirika la afya duniani. Ilipatwa Februari 21 2020.
 12. “2019-n-CoV: Kile ambacho umma inafaa kufanywa” Kituo cha kuzuia magonjwa Marekani. Februari 4 2020. Ilipatwa Februari 5 2020.
 13. “Ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19) ushauri kwa umma: Linin a jinsi ya kutumia barakoa.” Shirika la afya duniani. Shirika la afya duniani. 2020. Ilipatwa Aprili 6 2020
 14. "2019-nCoV: What the Public Should Do". US Centers for Disease Control and Prevention. 4 February 2020. Retrieved 5 February 2020.
 15. Jiji la Cameroon limeweka uvaliaji wa barakoa kuwa lazima ilikupigana na virusi vya corona. Taarifa za VOA. Aprili 7 2020
 16. Tasamba James (Aprili 19 2020). “Rwanda, Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo waweka uvaliaji wa barakoa kuwa lazima.”
 17. Samuel, Gelila (Aprili 12 2020). “Ethiopia wapiga marufuku kusalimiana kutumia mikono, inalazimisha uvaliaji wa barakoa kwenye maeneo ya umma.”
 18. Masilela, Brenda (Aprili 14 2020). Rais wa Guinea awekauvaliaji wa barakoa hadharani kuwa lazima ilikuwacha usambaji wa virusi wa corona” IOL
 19. Muraya, Joseph ( Aprili 5 2020) “Kenya: Barako ani lazima katika maeneo ya umma, Kenya yasema.” Afrika Yote
 20. Senkpeni, Alpha Daffae ( Aprili 21 2020). “Je, utavalia barakoa? Wanasheria wa Liberia wanataka uvaliaji wa barakoa katika umma iwe ni lazima.” Ukurasa wa kwanza Africa
 21. Elijechtimi, Ahmed ( Aprili 6 2020). “ Morocco yaweka uvaliaji wa barakoa kuwa lazima kwa sababu ya virusi vya corona” . Kituo cha Habari cha Uingereza. Ilipatwa Aprili 11 2020.
Rod of Asclepius2.svg Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Barakoa katika janga la corona 2019-20 kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.