Banguko
Jump to navigation
Jump to search
Banguko la mawe lililoharibu kijiji Puerto Rico
Banguko (ing. avalanche[1]) ni kiasi kikubwa cha theluji au barafu, pia cha mawe au ardhi, kinachoanza kusogea kwenye mtelemko wa mlimani na kuteleza au kuanguka kwa kuelekea bondeni.
Mwendo wa masi kubwa inaweza kusukuma miamba, miti na chochote kilichopo njiani kwenye mtelemko wa mlima na kuongeza banguko.
Banguko ni hatari kwa watu waliopo mlimani na pia kwa vijiji bondeni ambavyo vinafikiwa na banguko kubwa.
Katika Alpi za Ulaya takriban watu 100 hufariki kila mwaka kutokana na banguko.
Kwenye Andes za Peru watu 4,000 waliuawa na banguko kubwa tar. 11 Januari 1962. Banguko ya theluji ilitelemka mlima Huascaran na kufunika mji wa Yungay; mengine yalianguka katika mto na kusababisha mafuriko.
- Tazama pia: Miporomoko ya ardhi