Baldocchi
Mandhari
| Baldocchi | |
| Amezaliwa | 14 Machi 1946 Batatais, Brazil |
|---|---|
| Nchi | Brazil |
| Urefu | 1.89 m |
José Guilherme Baldocchi (alizaliwa 14 Machi 1946), anayejulikana zaidi kama Baldocchi, ni mchezaji wa zamani wa mpira wa miguu kutoka nchini Brazil aliyecheza nafasi ya beki wa kati.[1]
Katika ngazi ya klabu, alizichezea Batatais (1964–65), Botafogo-SP (1964–67), Palmeiras (1967–72), Corinthians (1971–75) na Fortaleza (1974–77). Alitwaa ubingwa wa Kombe la Brazil (Taça Brasil) mnamo mwaka 1967.[1]
Alicheza mechi moja ya kimataifa katika timu ya taifa ya Brazil, mnamo 4 Machi 1970 dhidi ya Argentina. Hata hivyo, alijumuishwa katika kikosi cha Brazil kilichotwaa ubingwa wa Kombe la Dunia la FIFA mwaka 1970.[1]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]| Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Baldocchi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |