Bakari (kundinyota)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Nyota za kundinyota Bakari (Bootes) katika sehemu yao ya angani

Bakari ( Bootes kwa Kilatini na Kiingereza) [1] [2]. ni jina la kundinyota kwenye nusutufe ya kaskazini ya dunia yetu.

Mahali pake[hariri | hariri chanzo]

Bakari iko kati ya kundinyota za Nadhifa (Virgo) na Dubu Mkubwa (Great Bear). Njia Nyeupe inapita katika sehemu ya Bakari.

Jina[hariri | hariri chanzo]

Bakari ilijulikana kwa jina hili kwa miaka mingi kati ya mabaharia Waswahili waliotumia nyota kutafuta njia baharini wakati wa usiku.[3]

Jina Bakari latokana na ar. بقار bakar yaani “mchunga ng’ombe”. Waarabu walipokea jina hili kutoka kwa elimu ya Wagiriki wa Kale. Mitholojia ya Kigiriki iliona hapa picha ya Philomelos mwana wa mungu wa kilimo Demeter aliyebuni plau inayovutwa na maksai. Kwa hiyo Bakari ni yule anayeongoza maksai wanaovuta plau.

Kuna pia majina tofauti kwa kundinyota hii ambayo yanarejelea mitholojia ambako shujaa wa kale alivinda dubu (kundinyota jirani kwenye anga).

Bakari-Bootes ni kati ya kundinyota zilizotajwa tayari na Klaudio Ptolemaio katika karne ya 2 BK. Iko pia kati ya kundinyota 88 zinazoorodheshwa na Umoja wa kimataifa wa astronomia [4]

Nyota[hariri | hariri chanzo]

Nyota angavu zaidi ni Simaki (α Alfa Bootis) inayojulikana pia kwa jina la kimataifa ya en:Arcturus yenye uangavu unaoonekana wa −0.05 mag ikiwa na umbali wa Dunia wa miaka ya nuru 36.7 (sawa na 11.26 parsek). Simaki ni nyota angavu zaidi ya nne angani.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Tahajia ya Bootes kwa Kiingereza mara nyingi ni “Boötes “ kwa kudokeza ya kwamba hapa hakuna “oo” ndefu “kama kwenye neno “ndoo” lakini “o-o” yaani sauti ya “o” mara mbili pekee. )
  2. Uhusika milikishi (en:genitive) ya neno "Bootes" katika lugha ya Kilatini ni "Bootis" na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Bootis, nk.
  3. ling. Knappert 1993
  4. The Constellations, tovuti ya International Astronomical Union , iliangaliwa Julai 2017

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Richard Hinckley Allen: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, ukurasa 75 ff (online hapa kwenye archive.org)
  • Jan Knappert, 1993: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331
Science-symbol-2.svg Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Bakari (kundinyota) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Science-symbol-2.svg Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Bakari (kundinyota) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.