Nenda kwa yaliyomo

Utawala wa Bahai

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Baháʼí administration)

Utawala wa Baháʼí ni mfumo wa asasi za kuchaguliwa na kuteuliwa kusimamia masuala ya jamii ya Kibaháʼí. Asasi ya juu kabisa ni Nyumba ya Haki ya Ulimwengu, inayochaguliwa kila baada ya miaka mitano.[1]

Baadhi ya sifa zinazotofautisha utawala wa Kibaháʼí na mifumo mingine ya utawala: wawakilishi waliochaguliwa wanapaswa kufuata dhamiri zao, badala ya kuwa na jukumu kwa maoni ya wapiga kura; kampeni za kisiasa, uteuzi na vyama vinakatazwa; na muundo na mamlaka ya asasi za kuongoza Wabaháʼí umetoka moja kwa moja kwa mwanzilishi wa dini hiyo, Baháʼu'lláh.

Utawala wa Kibaha'i unaongozwa na nyaraka nne za msingi, Kitáb-i-Aqdas, Nyaraka za Mpango Mtakatifu, Waraka wa Karmeli na Wasia na Agano la ʻAbdu'l-Bahá.[2][3][4]

Mashauriano

[hariri | hariri chanzo]

Jambo kuu na la kipekee katika utawala wa dini ya Kibaháʼí ni mtazamo wa kufanya maamuzi kupitia mashauriano. Lengo kuu la mashauriano ni kutafuta ukweli kwa pamoja na kuchunguza uhalisia kwa njia inayodumisha umoja na makubaliano.[5] ʻAbdu'l-Bahá aliwahimiza wajumbe waliochaguliwa "kufanya mashauriano kwa njia ambayo hakuna nafasi ya chuki au mfarakano itakayotokea."[6] Wabaháʼí wanahimizwa kutoa maoni yao kwa uwazi na utulivu katika mashauriano, wakijitenga kutokana na fikra zao wenyewe na kusikiliza mitazamo ya wengine bila upendeleo. Baada ya mashauriano ya kina juu ya mada fulani, ikiwa uamuzi mmoja wa pamoja hautofikiwa, uamuzi unaweza kufanywa kwa kufuata kura ya wengi.[7]

Mchoro wa mpangilio wa sasa wa utawala wa Kibaháʼí

Utawala wa Kibaháʼí unajumuisha asasi zilizochaguliwa na kuteuliwa. Vyombo vya uongozi vinavyoundwa na wajumbe tisa huchaguliwa kila mwaka katika ngazi ya mahali (mji, kijiji) na taifa, na kila baada ya miaka mitano wajumbe wa Mabaraza ya Kiroho ya Kitaifa hukusanyika kuchagua Nyumba ya Haki ya Ulimwengu, chombo cha uongozi cha kimataifa chenye mamlaka ya kuongeza na kutekeleza sheria za Baháʼu'lláh.[8][9] Asasi zinazoteuliwa katika mpangilio wa utawala wa Kibaháʼí ni pamoja na Kituo cha Ufundishaji cha Kimataifa, Bodi za Washauri wa Bara, na Bodi za Washauri Wasaidizi.[10]

Kwa vile hakuna makasisi katika Dini ya Kibahá'í, utawala wa Kibahá'í hufanya kazi kupitia aina ya serikali inayojisimamia yenyewe isiyo na mgawanyiko wa vyama vinavyokizana. Watu wanaochaguliwa kuhudumu katika taasisi za jamii ya Kibahá'í hawana mamlaka kama watu binafsi, ni chombo kilichoteuliwa tu ndicho kinachofanya maamuzi. Vivyo hivyo, watu ambao wanateuliwa kuhudumu katika nafasi za asasi pia "hawana mamlaka ya kutunga sheria, utekelezaji wa maamuzi, au mamlaka ya kimahakama", na badala yake wanatoa ushauri, faraja, na msaada kwa watu binafsi katika jamii na kwa asasi zilizochaguliwa.[11]

Mtu binafsi, jumuiya na asasi huchukuliwa kuwa manguli ambao wana majukumu tofauti tofauti ambayo yanasaidiana kwa pamoja katika kupiga hatua kwenye maendeleo.[12]

Mbinu ya uchaguzi

[hariri | hariri chanzo]
Wabaháʼí wa Kivietinamu wakichagua Baraza lao la Kiroho la Kitaifa huko Danang, mwaka 2009.

Mabaraza ya Kiroho ya Mahali huchaguliwa kila mwaka siku ya kwanza ya Ridván (kawaida tarehe 20 au 21 Aprili). Wajumbe tisa wa Baraza la Kiroho la Mahali huchaguliwa kwa kura ya siri bila mchakato wa kampeni au uteuzi. Kwa ujumla, Wabaháʼí wote watu wazima waliosajiliwa katika jamii wanastahili kushiriki kwenye uchaguzi na pia wanastahili kuchaguliwa. Kila mtu huandika kwenye karatasi yake ya kura majina ya watu tisa katika jamii ambao wanaona wanaonyesha vyema "sifa zinazohitajika za uaminifu usio na shaka, kujitolea bila ubinafsi, akili iliyofunzwa vyema, uwezo unaotambulika na uzoefu uliopevuka."[13] Ili kuamua nani wa kumpigia kura, Wabaháʼí wanahimizwa kujifahamisha kikamilifu wao kwa wao, kubadilishana mawazo, na kujadili kwa uhuru mahitaji na sifa za huduma kwenye asasi; hata hivyo, hii inapaswa kufanywa bila hata kupendekeza watu mahususi.[14]

Katika ngazi ya kitaifa, mchakato wa uchaguzi wa hatua mbili hutumika. Katika kila eneo la uchaguzi ndani ya nchi, waumini wa jamii huchagua kila mwaka idadi maalum ya wawakilishi, ambao wanagawanywa kwa uwiano kulingana na idadi ya watu wa kila eneo la uchaguzi, na wawakilishi hawa hukusanyika katika Mkutano wa Kitaifa ili kuchagua wajumbe wa Baraza la Kiroho la Kitaifa. Vivyo hivyo, kila baada ya miaka mitano wajumbe wa kila Baraza la Kiroho la Kitaifa hukusanyika katika Mkutano wa Kimataifa kuchagua wajumbe wa Nyumba ya Haki ya Ulimwengu.[13]

Kutokuwa wa Upande

[hariri | hariri chanzo]

Shoghi Effendi alikemea vikali siasa za vyama na mbinu nyingine za kisasa zinazofanywa katika demokrasia za magharibi, kama vile kampeni za kisiasa na uteuzi. Matokeo yake:[15]

  • Uteuzi na kampeni zimepigwa marufuku. Wabaháʼí hawapaswi kujitafutia nafasi kama wagombea.
  • Wapiga kura wanahimizwa kutoshauriana kuhusu ufaaji wa watu fulani.
  • Wapiga kura wanapaswa "kubadilishana maoni... kuchangamana kwa uhuru na kujadili baina yao wenyewe mahitaji na sifa" za ujumbe katika asasi. Hata hivyo, mjadala haupaswi kuwahusu watu binafsi.
  • Wapiga kura wanahimizwa sana kusoma na kujadili, kwa namna ya jumla, sifa zilizoainishwa na Shoghi Effendi kuwa muhimu kwa wale wanaochaguliwa kuhudumu, bila kurejelea watu binafsi. Sifa hizo ni “uaminifu usiopingika, kujitolea bila ubinafsi, akili iliyofunzwa vyema, uwezo uliotambuliwa na uzoefu uliokomaa” na kuwa “waaminifu, wakweli, wenye uzoefu, wenye uwezo na stadi”.
  • Mpiga kura anapaswa kuchukua hatua "bila chembe ya shauku au ubaguzi wowote, na bila kujali masuala yoyote ya kimwili”

Taasisi zilizochaguliwa

[hariri | hariri chanzo]

Wakati mwingine hurejelewa na Baháʼu'lláh kama "Watawala", Wabaháʼí huchagua wajumbe wa mabaraza ambayo yanakabidhiwa mamlaka ya jamii. Wajumbe wa mabaraza haya, wenyewe, hawana mamlaka ya kibinafsi. Hata hivyo, yanapoundwa ipasavyo, na hasa yanapoamua mambo kama chombo, mabaraza haya hutenda kama viongozi wa jamii.[16] Baháʼu'lláh aliongelea Nyumba ya Haki ya Ulimwengu, pamoja na Nyumba za Haki za mahali katika kila jamii ambapo Wabaháʼí watu wazima tisa au zaidi wanaishi. ʻAbdu'l-Bahá alifunua juu ya "Sekondari", au Nyumba ya Kitaifa ya Haki katika wosia wake. Zikichukuliwa kama asasi ambazo bado zinakua, Nyumba za Haki za Kitaifa na za Mahali kwa sasa zimepewa jina la muda la "Mabaraza ya Kiroho"[16] na zinatarajiwa, baada ya muda, kukomaa kuwa Nyumba za Haki zinazofanya kazi kikamilifu.

Nyumba ya Haki ya Ulimwengu inachukuliwa kuwa isiyokosea kimaadili, ingawa imani hii ina maelezo madogo madogo, kwa kuwa Nyumba ya Haki ya Ulimwengu inaweza kuanzisha sheria mpya za Kibaháʼí na kufuta sheria zake yenyewe. Haitakiwi kubadilisha sheria za maandiko zilizowekwa na Baháʼu'lláh na ʻAbdu'l-Bahá. Mabaraza ya Kitaifa na ya Kiroho ya Mahali yanahitaji heshima na utiifu, lakini maamuzi yake yanaweza kutenguliwa na asasi ya juu yake iliyochaguliwa. Maamuzi yote ya mabaraza haya lazima yafanywe, na yanachukuliwa kuwa halali ikiwa, na tu ikiwa chombo hicho kimeundwa ipasavyo, na kinakutana kama chombo chenye idadi ya kutosha ya washiriki waliopo. Maamuzi haya hufanywa kupitia mchakato maalum wa ushauriano.

Nyumba ya Haki ya Ulimwengu

[hariri | hariri chanzo]
Makao ya Nyumba ya Haki ya Ulimwengu huko Haifa, Israeli

Kila baada ya miaka mitano kuanzia 1963, wajumbe wa Mabaraza yote ya Kiroho ya Kitaifa hualikwa kupiga kura katika Mkutano wa Kimataifa katika Kituo cha Ulimwengu cha Wabaháʼí huko Haifa, Israeli kwa ajili ya wajumbe wa Nyumba ya Haki ya Ulimwengu.[17] Hawa wajumbe hufanya kazi kama wawakilishi kwa njia inayofanana na uchaguzi wa Kitaifa wa WaBaháʼí. Wale ambao hawawezi kuhudhuria hutuma kura zao.[18]

Nyumba ya Haki ya Ulimwengu ni chombo kikuu cha utawala cha Dini ya Kibaháʼí. Maandiko ya Kibaháʼí yanathibitisha kwamba maamuzi yake ni "chanzo cha wema wote na yameepushwa na makosa yote".

Mabaraza ya Kiroho ya Kitaifa

[hariri | hariri chanzo]

Baraza la Kiroho la Kitaifa (NSA) kawaida linaashiria nchi, ingawa wakati mwingine maeneo hupewa NSA zao (km. Alaska). Wakati mwingine nchi kadhaa hukusanywa pamoja kuunda Baraza moja, kwa mfano Nchi za Baltiki, au (awali) Kanada na Marekani. Mipaka hii inategemea mamlaka ya Nyumba ya Haki ya Ulimwengu, na inaweza kubadilika; Kanada na Marekani sasa wana mabaraza yao ya kitaifa yanayojitegemea. Mabaraza haya huchaguliwa kila mwaka kupitia wawakilishi walioteuliwa kwa uchaguzi wa mahali.[19]

Mabaraza ya kitaifa (au mabaraza ya kikanda) huteua kamati na bodi mbalimbali kutekeleza kazi mbalimbali: Bodi za Taasisi za Kikanda, Kamati za Ufundishaji za Eneo, Wasaidizi wa Ukuaji wa Klasta, Waratibu wa Taasisi za Klasta, Waratibu wa Programu ya Uwezeshaji wa Kiroho kwa Vijana Wadogo wa Klasta, na Mratibu wa Madarasa ya Watoto wa Klasta wakiwa mifano.

Halmshauri za Kanda za Kibaháʼí

[hariri | hariri chanzo]

Halmashauri za Kikanda za Kibaháʼí (RBC) pia zimeanzishwa katika baadhi ya jumuiya kubwa za kitaifa za Kibaháʼí kama ngazi ya kati ya utawala kati ya mabaraza ya kiroho ya kitaifa na ya mihali ili kuwezesha kufanya maamuzi kwa njia iliyogatuliwa pale inapohitajika. Hii hutokea mara nyingi nchi inapokuwa kubwa sana (kwa mfano, Marekani, India na hata Tanzania). Yanashirikiana chini ya uongozi wa Baraza la Kiroho la Kitaifa na huchaguliwa na wajumbe wa Mabaraza ya Kiroho ya Mahali katika kanda zao. Majukumu yao yanatanuka na hushiriki katika shughuli za ukuaji wa jumuiya na maendeleo, na yanatoa mwongozo na muundo kwa uratibu wa jumuiya za mahali katika kanda zao.[19]

Mabaraza ya Kiroho ya Mahali

[hariri | hariri chanzo]

Mabaraza ya Kiroho ya Mahali (LSA) yanawakilisha mji, jiji, au kata, na huchaguliwa kila mwaka kupitia uchaguzi wa moja kwa moja. Mabaraza ya Mahali yanasimamia maisha ya jamii ya Wabahá'í katika ngazi ya mahali, na kusimamia shughuli za jamii nzima, ikiwemo kuratibu Karamu ya Siku Kumi na Tisa, maadhimisho ya siku takatifu, huduma za mazishi, ushauri wa ndoa na kazi nyingine nyingi, ingawa kwa kawaida hizi hufanywa kupitia kamati zilizoteuliwa.[19]

Taasisi za kuteuliwa

[hariri | hariri chanzo]

Baháʼu'lláh huwataja "wasomi" miongoni mwa watu wake. Majukumu ya mkono huu awali yalitekelezwa na Mikono wa Hoja wa Mungu walioteuliwa na Baháʼu'lláh, ʻAbdu'l-Bahá, na Shoghi Effendi. Ilipobainika kuwa hakuna "Mikono" zaidi wangeweza kuteuliwa, Nyumba ya Haki ya Ulimwengu iliunda Asasi ya Washauri kutekeleza majukumu yao. Wajumbe walioteuliwa hufanya kama watu binafsi na jukumu lao kubwa ni la kutia moyo na kushauri. Majukumu yao yamegawanywa katika makundi mawili makuu ya ulinzi na uenezaji wa Dini ya Kibaháʼí.[20]

Washauri wa Kimataifa

[hariri | hariri chanzo]

Washauri wa Kimataifa ni watu tisa walioteuliwa katika Kituo cha Ufundishaji cha Kimataifa, ambacho ni chombo kinachosaidia moja kwa moja Nyumba ya Haki ya Ulimwengu katika Kituo cha Ulimwengu cha Wabaháʼí. Wanawashauri Wabaháʼí katika kiwango cha kimataifa na kuratibu juhudi za Washauri wa Bara.[21]

Washauri wa Bara

[hariri | hariri chanzo]

Washauri binafsi wanapewa jukumu katika Bodi za Bara, ambapo wanashirikiana moja kwa moja na Mabaraza kadhaa ya Kiroho ya Kitaifa. Mara nyingi hufanya kazi katika uwezo wa kutoa taarifa, wakielezea maelekezo na majadiliano kutoka Kituo cha Ulimwengu na jumuiya za kitaifa. Mara nyingi hujikita kazi yao katika nchi moja au seti ya nchi ndani ya eneo lao la utendaji.[21]

Bodi ya Washauri Wasaidizi

[hariri | hariri chanzo]

Bodi ya Washauri Wasaidizi huteuliwa na Washauri wa Bara ili kuwasaidia katika maeneo madogo zaidi ya kijiografia. Hufanya kazi na Mabaraza yoyote ya Kiroho ya Mahali, Halmashauri za Kanda, na watu binafsi ndani ya maeneo yao ya utendaji. Kwa kawaida kuna washauri wasaidizi mawili katika eneo moja la kijiografia, moja aliye na jukumu la ulinzi, na mwingine la kupanua jamii, ingawa kazi hizi mara nyingi huingiliana. Washauri wote wawili huripoti kwa Bodi ya Washauri wa Bara iliyowateua, bila kujali eneo lao la utendaji.[22]

Wasaidizi

[hariri | hariri chanzo]

Washauri wasaidizi huteua "wasaidizi" wanaofanya kazi kwa niaba yao katika ngazi za ughani. Wasaidizi hawa mara nyingi hukutana na Mabaraza ya Kiroho ya Mahali, huzungumza kwenye matukio, na hutafutwa kwa ushauri na muumini mmoja mmoja. Wakati mwingine watakuwa na jukumu katika eneo maalum, kama vile kuangazia vijana katika jiji fulani, au wanaweza kuteuliwa kwa ujumla. Wajibu wao ni wa kubadilika kulingana na jinsi mshauri msaidizi anavyohisi inafaa.[22]

Msingi wa Kihistoria

[hariri | hariri chanzo]

Wakati wa maisha ya Baháʼu'lláh

[hariri | hariri chanzo]

Maelezo ya mwanzo ya usimamizi unaofanya kazi ndani ya jamii ya Wabahá'í duniani kote yanapatikana katika maandiko ya Baháʼu'lláh. Yameanzishwa kwa imani kwamba Mungu huwaongoza wanadamu kupitia watume, wengi wao wamebashiri "Ufalme wa Mbingu duniani", na imani kwamba ufunuo wa Baháʼu'lláh ni utimilifu wa unabii huo, Wabahá'í wanaona katika maandiko yake mfumo wa Mungu na wa watu.

Ingawa Baháʼu'lláh alibainisha, awali, sera nyingi ambazo zingekuwa msingi wa mfumo wa kiutawala wa Kibahá'í, kitabu chake Kitáb-i-Aqdas kinatoa mwangaza wa awali thabiti wa mfumo huu:

"Bwana ameagiza kwamba katika kila mji iwepo Nyumba ya Haki ambapo watakusanyika washauri kwa idadi ya Bahá, na iwapo itazidi idadi hii haitajalisha. Wanapaswa kujiona kama wanaingia katika Mahakama ya uwepo wa Mungu, Aliyetukuka, Aliye Juu Zaidi, na kama wanamtazama Yeye Aliye Asiyeonekana. Inawapasa kuwa watu wa kuaminiwa miongoni mwa watu na kujiona kama walinzi walioteuliwa na Mungu kwa ajili ya wote wanaoishi duniani. Ni wajibu wao kushauriana na kuzingatia maslahi ya watumishi wa Mungu, kwa ajili Yake, kama wanavyozingatia maslahi yao wenyewe, na kuchagua kile kilicho bora na kinachofaa."[23]

Baada ya muda, dhana hizi zilifafanuliwa awali katika maandiko ya Baháʼu'lláh, na kisha katika maandiko ya mwanawe mkubwa na mrithi wake, ʻAbdu'l-Bahá.

Utumishi wa ʻAbdu'l-Bahá

[hariri | hariri chanzo]

Ni ʻAbdu'l-Bahá ambaye alibainisha majukumu tofauti ya Nyumba za Haki za Juu/Ulimwengu(dunia) dhidi ya za Mahali. Wakati wa maisha ya ʻAbdu'l-Bahá, alisimamia na kuhimiza kuanzishwa kwa mabaraza mengi ya Mahali yaliyochaguliwa, akiyaita "Mabaraza ya Kiroho". Aliandika barua nyingi za kufafanua, akitoa maelekezo kwa Mabaraza mbalimbali ya Kiroho, akiipa dunia ya Kibaháʼí msukumo. Nyaraka za Mpango Mtakatifu zina nafasi ya kipekee, na zimekuwa kwa kiwango kikubwa zikiongoza mchakato wa upangaji wa malengo wa awali wa jamii hii changa ya kiroho. Mpango huu ulifungua maeneo mapya kabisa ya kijiografia kwa Wabaháʼí, ʻAbdu'l-Bahá akihimiza Wabaháʼí kuungana na watu wa rangi na tamaduni zote.

Moja ya urithi wake mkubwa kwa maendeleo ya mfumo wa utawala wa Kibaha'i, hata hivyo, ilikuwa wosia na agano lake, ambapo anaelezea taasisi kadhaa mpya. Akifafanua maoni ya Baháʼu'lláh kuhusu vizazi vyake na mamlaka, alielezea Asasi ya Ulinzi, ambayo aliiona ikifanya kazi kwa pamoja na Nyumba ya Haki ya Ulimwengu – moja ikiwa na jukumu la kutafsiri maandiko, nyingine kama mtungaji wa sheria mpya ambazo hazijashughulikiwa na maandiko yaliyopo. Kwa haya aliamuru utiifu wa Wabaháʼí.

"Tawi takatifu na changa, Mlinzi wa Dini ya Mungu, pamoja na Nyumba ya Haki ya Ulimwengu itakayochaguliwa na kuimarishwa kikamilifu, zote ziko chini ya uangalizi na ulinzi wa Uzuri wa Abhá, chini ya hifadhi na mwongozo usiokosea wa Yule Aliyeinuliwa (maisha yangu yatolewe kwa ajili yao wote wawili). Lolote watakaloamua ni la Mungu. Yeyote asiyetii yeye, wala asiyetii wao, hajamtii Mungu; yeyote anayeasi dhidi yake na dhidi yao amemuasi Mungu; yeyote anayewapinga amempinga Mungu; yeyote anayebishana nao ameshibishana na Mungu; yeyote anayebishana naye amebishana na Mungu"[23]

Katika waraka huu, ʻAbdu'l-Bahá pia:

  • alimteua mjukuu wake Shoghi Effendi kuwa Mlinzi wa Dini ya Mungu.
  • aliweka vigezo vya kuteua Walinzi wa baadaye.
  • alifafanua upeo mpya wa asasi ya kuchaguliwa aliyoiita "Nyumba ya Haki ya Pili", ambazo za kwanza zilichaguliwa chini ya usimamizi wa Shoghi Effendi.
  • aliwaagiza waumini kuepuka Mvunjaji wa Agano – Wabaháʼí waliopinga mkuu wa imani na kujaribu kuunda mgawanyiko au kundi.
  • alibainisha baadhi ya masharti kwa ajili ya maendeleo ya baadaye ya utawala wa Wabaháʼí.
  • alifafanua taasisi ya Mikono wa Hoja, na kufafanua mahitaji ya uteuzi wao.

Utumishi wa Shoghi Effendi

[hariri | hariri chanzo]
Mahali alipopumzika Shoghi Effendi huko London katika Makaburi ya New Southgate

Chini ya Shoghi Effendi, Dini ya Kibaháʼí ilipitia mabadiliko makubwa sana katika umbo na mchakato wake. Wakati wa kuendeleza kutoka muundo wa msingi uliowekwa na Baháʼu'lláh na ʻAbdu'l-Bahá, Shoghi Effendi alianzisha kampeni kubwa-kubwa za kuimarisha utawala, alianzisha taratibu na michakato kwa vyombo vya utawala vya Kibaháʼí, aliteua Mikono wa Hoja zaidi, alihakikisha kutambulika kwa nafasi ya kisheria ya Jumuiya ya Kibaháʼí huko Haifa, lakini pia, akifanya kazi na Mabaraza ya Kiroho ya Kitaifa mapya yaliyoundwa, na serikali nyingi za kitaifa. Katika kipindi hiki, asasi za Kibaháʼí na ushirikiano kati ya asasi ulikuwa wazi zaidi, mambo mengi ya sheria ya Kibaháʼí yalielezwa, na imani ilienea sehemu nyingi za dunia. Ndoa za Kibaháʼí zilitambuliwa kuwa halali katika kanda kadhaa na Dini ya Kibaháʼí ilitambuliwa kama dini inayojitegemea na mataifa mengi na mahakama za kidini, ikijumuisha mahakama za kidini za Kiislamu huko Misri. Shoghi Effendi alielezea kifo cha ʻAbdu'l-Bahá na mwanzo wa utawala wake mwenyewe kama mwisho wa "Zama za Kishujaa" na mwanzo wa Zama ya "Uundaji" ya Dini ya Kibaháʼí.

Mageuzi ya kisasa

[hariri | hariri chanzo]

Miaka mia moja baada ya kifo cha Baháʼu'lláh, Wabaháʼí waliadhimisha "mwaka mtakatifu", ambapo tafsiri kamilifu iliyoidhinishwa ya Kitáb-i-Aqdas (Kitabu Kitakatifu Zaidi) ilichapishwa, ikiambatana na utumikaji ulioongezeka wa sheria za Kibaháʼí miongoni mwa Wabaháʼí wasio Wairani na ukomavu wa Mabaraza ya Kiroho.

Mnamo mwaka wa 1997, Nyumba ya Haki ya Ulimwengu ilianzisha Halmashauri za Kanda za Kibahai katika nchi mbalimbali (kwa mfano Marekani, Kanada, India, Tanzania) ili kuwepo na chombo cha kati cha utawala kati ya Mabaraza ya Kiroho ya mahali na kitaifa.[onesha uthibitisho]

Mwandishi wa habari na mwandishi Amanda Ripley katika kitabu chake cha 2021 High Conflict: why we get trapped and how we get out, anaelezea mfumo wa uchaguzi na utawala wa Wabahá'í akisema "…kila kitu kuhusu uchaguzi huu kimeundwa kupunguza uwezekano wa migogoro mikubwa." Kwa hakika kwamba "Wabahá'í wanajaribu kuchagua watu ambao hawapendelei sifa na madaraka." na "Katika kila mkutano, wanafuata utaratibu unaoitwa 'kushauriana,' ambao umeundwa ili kuruhusu watu kusema maoni yao bila kushikilia katika ushawishi wao wenyewe." Kwa muhtasari wa Ripley "Kama wanasosholojia wangeunda dini, ingeonekana kama hii.… Kwa njia hii, uchaguzi wa KiBaha’i ume…undwa kutumia uwezo wa binadamu wa kushirikiana, badala ya kushindana."[24]

  1. Smith 2000, pp. 24–29, Administration.
  2. Phelps 2021, p. 71.
  3. Yazdani 2021, p. 92.
  4. Danesh 2021, p. 363.
  5. Danesh 2021, pp. 449–454.
  6. Adamson 2006, p. 108.
  7. Momen 2005.
  8. Smith 2000, pp. 346–350, Universal House of Justice.
  9. Danesh 2021, pp. 426–429.
  10. Danesh 2021, p. 430.
  11. Danesh 2021, pp. 426–430.
  12. Danesh 2021.
  13. 1 2 Danesh 2021, pp. 436–437.
  14. Abizadeh 2008, p. 78.
  15. Abizadeh 2008.
  16. 1 2 Fox 1998.
  17. Smith 2021, p. 138.
  18. Smith 2021, p. 136.
  19. 1 2 3 Smith 2008.
  20. Smith 2008, pp. 181–182.
  21. 1 2 Smith 2021b.
  22. 1 2 Smith 2008, p. 182.
  23. 1 2 Vafai 2021, p. 12.
  24. Ripley 2022, pp. xi, 91–5.
  • Abizadeh, Arash (2008-12-01). "Jinsi Wapiga Kura wa Bahá'í Wanavyopaswa Kupiga Kura". The Journal of Bahá'í Studies (kwa Kiingereza). 18 (1–4): 77–94. doi:10.31581/jbs-18.1-4.3(2008). ISSN 2563-755X.
  • Adamson, Hugh C. (2006-12-21). Historical Dictionary of the Baha'i Faith. Scarecrow Press. ISBN 978-0-8108-6467-2.
  • MacEoin, Denis (1997). Hinnells, John R. (mhr.). Muongozo Mpya wa Dini Zinazoishi. Blackwell Publishers. ISBN 0-631-18275-6.
  • Mitchell, Glenford E. (2009). "Utawala, Baháʼí". Mradi wa Baháʼí Encyclopedia. Evanston, IL: Bunge la Kiroho la Kitaifa la Wabaháʼí wa Marekani.
  • Smith, Peter (2000). Ensaiklopidia Fupi ya Dini ya Baha'i. Oxford: Oneworld Publications. ISBN 1-85168-184-1.
  • Smith, Peter (2008). Utangulizi wa Dini ya Baha'i. Cambridge: Chuo Kikuu cha Cambridge. ku. 178–9. ISBN 978-0-521-86251-6.

Marejeleo ya ziada

[hariri | hariri chanzo]