Bada

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Bada ni ugali wa muhogo, ni ugali mweusi. Ni chakula cha asili cha jamii mbalimbali za Kitanzania, chakula hiki hutengenezwa kutokana na muhogo.

Kwanza mihogo inapovunwa hukaushwa, halafu baada ya kukauka hupondwapondwa kwenye kinu au kusangwa kwenye mashine mpaka upatikane unga.

Namna ya kuupika ni kwamba, kwanza unaweka maji jikoni mpaka yachemke halafu unatia unga na kuanza kusonga.

Kinachoshangaza ni kwamba unapoanza kusonga na ugali unapoanza kuwa mgumu jikoni ndipo hapo hapo unaanza kuwa mweusi hapo ndipo unapopata ugali unaoitwa bada.

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Bada kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.