Nenda kwa yaliyomo

Azeline Hearne

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Azeline Hearne (takriban 1825–1890?) alikuwa mwanamke Mmarekani aliyekuwa mtumwa na baadaye aliachiliwa akiwa katika miaka yake ya 30. Alijulikana kutokana na kesi nyingi za kisheria zilizofunguliwa dhidi yake wakati wa kipindi cha Ujenzi Mpya baada ya Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Marekani.

Kwa muda mfupi, Hearne alikuwa miongoni mwa wamiliki matajiri zaidi wa ardhi huko Texas, lakini baadaye alipoteza mali yake na kuishi katika umaskini kutokana na kesi za madai ambazo wanahistoria wa kisasa wameziona kuwa zisizo za haki.

Wakati akiwa mtumwa, Azeline aliishi pamoja na mmiliki wake mzungu wa utumwa, Samuel R. Hearne, na wakapata watoto wanne.

Mwaka 1853, familia ya Hearne ilihamia Kaunti ya Robertson, Texas.

Samuel Hearne alipofariki mwaka 1866, aliacha mali yake kwa mtoto wao wa kiume mwenye umri wa miaka 20, kwa sharti kwamba amtunze Azeline.[1]

Mtoto huyo alipofariki baadaye katika mlipuko wa homa ya manjano mwaka 1868, Azeline, akiwa mrithi pekee, alirithi mali yake.

Urithi huo ulimfanya kuwa miongoni mwa wamiliki matajiri zaidi wa ardhi katika kaunti hiyo.

Aidha, Benjamin Brown, ambaye alipaswa kumsaidia kulinda mali zake, alifanya udanganyifu dhidi yake. Jambo hilo lilimfanya Azeline kuwa mlengwa rahisi wa watu weupe waliotaka kumnyang'anya mali yake.[2]

  1. ↑ Cynthia Hall Clements (2010-05-26). "Civil Wrongs". The Texas Observer (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2026-08-10.
  2. ↑ Howell, Kenneth Wayne (2012). Still the Arena of Civil War: Violence and Turmoil in Reconstruction Texas, 1865-1874 (kwa Kiingereza). University of North Texas Press. ISBN 978-1-57441-449-3.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Azeline Hearne kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.