Nenda kwa yaliyomo

Ayamase

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ayamase (pia huandikwa Ayamashe) ni aina maalumu ya mchuzi au kitoweo kinachotoka kwa Wayoruba kutoka Nigeria, Afrika Magharibi.[1] Huliwa pamoja na wali wa Ofada na wakati mwingine wali mweupe wa kawaida. Hutengenezwa kwa pilipili, pilipili hoho na viungo mbalimbali.[2][3]

Kwa kawaida hujumuisha nyama, samaki na mayai. [4]Ina rangi ya kijani iliyokolea. Hutofautiana na kitoweo kinachoitwa mchuzi wa Ofada au Lafenwa, ambacho huwa na rangi ya wekundu na pia huliwa pamoja na wali wa Ofada.[5]

Ayamase ni maarufu katika sherehe za Kiyoruba zinazoitwa Owanbe na pia hupikwa majumbani.

  1. Chichi Uguru (2018-01-17). "Ayamase Stew (Designer Green Pepper Stew/Ofada)". My Diaspora Kitchen (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2026-04-07.
  2. Sisi Jemimah (2015-08-04). "Ayamase - Ofada Stew". Sisi Jemimah (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2026-04-07.
  3. Lola Osinkolu (2025-04-07). "How to pepare Ayamase stew (ofada stew)". Chef Lola's Kitchen (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2026-04-07.
  4. Souldeliciouz (2014-11-01). "How to cook Ayamase (Designer and Ofada) Stew". SOULDELICIOUZ KITCHEN (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2026-04-07.
  5. Ajoke (2019-11-09). "Ayamase (Designer stew)". My Active Kitchen (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2026-04-07.