Axum

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 07:00, 11 Machi 2013 na Addbot (majadiliano | michango) (Bot: Migrating 49 interwiki links, now provided by Wikidata on d:q5832 (translate me))


Aksum
Aksum is located in Ethiopia
Aksum
Aksum

Mahali pa mji wa Aksum katika Ethiopia

Majiranukta: 14°7′N 38°44′E / 14.117°N 38.733°E / 14.117; 38.733
Nchi Ethiopia
Mkoa Tigray
Wilaya Mehakelegnaw
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 56,500
Karibu na Mashariki mwaka 565 AD, Ikionesha Ufalme wa Aksum na majirani zake

Axum au Aksum ni mji katika upande wa kaskazini mwa nchi ya Ethiopia. Hapa ndipo palipokuwa na Ufalme wa Aksum. Axum alikuwa ni mwanajeshi wa majini na mfanyabishara aliyeongoza sehemu hiyo tangu miaka 400, kabla ya Kristo, hadi katika karne ya 10. Pia katika kipindi cha mwanzo, eneo la ufalme wa Axum lilijulikana pia kama Abyssinia, Ethiopia na India katika maandishi ya kale.

Likiwa katika eneo la kanda ya Mehakelegnaw, katika moja ya maeneo ya Tigray, chini ya milima ya Adwa, mji wa Axum umeinuka kiasi cha mita 2,131. Mji wa Axum ulikuwa ni kituo cha dini ya Kikristo, jeshi la maji, shughuli za kibiashara, na nguvu za kimataifa za Ufalme wa Aksumite, ambao pia umeandikwa katika maandishi ya zamani yaliyopatikana nchini Rome katika kipindi cha kuzaliwa kwa Kristo, na pia yamehusishwa na kupanuka kwa mji wa Roma katika eneo la kaskazini mwa Afrikana baadae mji huo ukaendelea na kuwa falme wa dini ya Kikristu. Lakini kwa ujumla historia kamili ya mji huu bado haijafahamika, hadi hii leo chanzo halisi cha historia ya mji huu ni kutoka katika maandishi ya kanisa.

Inaaminika kuwa, mji huo ulianza kuanguka katika karne ya 7, kutokana na kuingiliwa na makundi ya waislamu waliokuwa wanapigania misafara ya kibiashara. Kwa hali hii, mji wa Aksum ulitengwa kutoka kutoka kwa misafara yake ya biashara ya Alexandria, Byzantium na Ulaya ya Kusini na sehemu yake ya biashara ilichukuliwa na wafanyabiashara wa Kiarabu wa kipindi hicho.

Ufalme wa Aksum, pia umekuwa katika hali ya kutopatana na makundi ya waislamu juu ya dini, hali iliyopelekea wakazi wa Aksumu kuhamia upande wa kusini na ustaarabu wa kuanza kuisha. Kutoka na kuangushwa kwa mamlaka ya Aksum, pia ushawishi wake ukaanza kupotea hali inayosemekana ilitokana na kupungua kwa idadi ya watu. Mfalme wa mwisho kuwahi kushika madaraka juu ya Aksum, aliwekwa madarakani katika karne ya kumi, lakini nguvu za utawala wa ufalme huu, ulianza kuisha hata kabla ya mfalme huyu.

Kutokana na kuanguka kwa nguvu na idadi ya watu katika ufalme wa Aksum, hii ilichangia kuhama kwa nguvu za utawala na kuhamisha ufalme wake katika Ufalme wa Ethiopia ili uweze kukua kwa haraka na hatimaye kuweza kurudisha hadhi yake ya mwanza, na hivyo kukaja nji uliotwa Ethiopia na hadi sasa ukabaki kuwa mji wa Ethiopia .[1]

Kutokana na Rekodi za Central Statistical Agencyya mwaka 2005, Axum una idadi ya watu wanaokadiriwa kufika 47,774 ambapo wanaume ni 20,774 na wakati wanawake ni 21,898.[2] Asilimia sabini na tano ya wakazi wa eneo hili ni waumini wa kanisa la kikristo lenye imani kali, Wengine wanaobaki ni waumini wa madhahebu ya Sunni Muslim na dhahebu la P'ent'ay

Aksum inatumia usafiri wa nndege na kutumia uwanja wa airport (ICAO code HAAX, IATA AXU).

Ufalme wa Aksumite na kanisa la Ethiopia

Dome na Belltower ya kanisa Jipya la Our Lady Mary of Zion
The Chapel of the Tablet

Ufalme wa Aksum una lugha yake yenyewe inayoitwa Ge'ez, na pia umeendeleza sanaa ya ujengaji majengokwa kutumia miamba kuanzaia miaka ya 5,000 hadi 2,000 kabla ya Kristu .[3]. Ufalme huu, ulifikia katika nafasi kubwa zaidi ya mafanikio mwaka chini ya mfalme Ezana aliyebatizwa kama Abreha, katika karne ya karne 4,miaka 300 baada ya kifo cha Yesu, hali inayoelezewa katika maandishi ya kikristo [4]

Mwaka 1937,nguzo yenye urefu wa mita 24 na yenye umri wa miaka 1700,iliyokuwa imelala ardhini, inayojulikana kamaObelisk of Axum ilivunjwa katika vipande viatani na kusafirishwa na wanajeshi wa Itali hadi nchini Itali na kupelekwa na kupelekwa katika eneo la Rome ili kusimamishwa. Nguzo hii inaamika kuwa ni moja kati vithibitisho vinavyoonesha ujenzi wa kutumia sayansi ya hali ya juu katika Ufalme wa Axumite.

Japokuwa umoja wa mataifa mwaka 1947, uliamuru kurudishwa kwa nguzo hiyo nchini Ethiopia, lakini Itali imekuwa ikikataa na kupelekea kusainiwa kwa mkatana juu ya nguzo hiyo, ianyoaminika mionagoni mwa wananchi wa Ethiopia kuwa ishara ya Utaifa wao

Hatimaye mwaka 2005, Nchi ya Itali ilimua kurudisha nguzo hizo nchini Ethiopia na kupokelewa na umati wa watu wakiwa na furaha, pia itali ililipa gharama zote za usafiri zilizogharimu kiais cha dola milioni nne. UNESCO ikabeba jukumu la kuzisimamisha nguzo hizo na kufikia mwezi Julai mwaka 2008, nguzo zote zilikuwa tayari zimesimama katika eneo la Axum. Sherehe za kupokea nguzo hizo zilifanyika katika jiji la Paris Tarehe 4 Septemba 2008, ambapo viongozi mbalimbali kutoka nchini Ufaransa na Ethipia walishiriki, ambapo waziri mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi, alizitoa kwa raisi wa Itali a kwa juhudi zake za kuzirudisha nguzo hizo nchini kwao

Axum na Waislamu

Ufalme wa Axum, unamahusiano ya muda mrefu na dini ya Islamu, According to ibn Hisham [5], wakati Muhammad alipota matatizo kutoka kwa koo ya Quraish alituma kundi dogo lililojumuisha mtoto wake wa kike Ruqayya na mumewe Uthman ibn Affan, ambaye mfalme wa Axum Ashama ibn Abjar, aliwapa makazi na ulinzi na kukataa maombi ya mfalme wao kutaka kuwarudisha kwao Arabia. [onesha uthibitisho] Mateka hawa hakurea hadi mwaka wa sita wa Hijra (628), na hata katika wakati huu, wengi walibakia nchini Ethiopia na hatimaye kuja kukaa katika eneo la Negash mashariki mwa Tigray.[onesha uthibitisho]

Kwa ujumla kina mifano kadhaa ikionesha, uwepo wa dini ya Uislamu na athari zake katika eneo la Axum. Utamaduni wa Waislamu ni kuwa, kiongozi wa Axum aliwapenda sana wageni waliokuwa katika eneo hili kwa kiasi cha kubadili dini kwa siri.[6] Kwa upande mwingine, Wanahistoria wa kiarabu, na wakazi wa Ethipia, baadhi ya wageni wa kiislamu walioishi nchini Ethipia, walibadilisha dini na kuwa wakristu

Maeneo ya Kuvutia

Kasakzini mwa Hifadhi ya, na majirani kwa zake kwa upande wa nyuma

Maeneo kadhaa yanavutia katika eneo la Aksum, Nguzo za Aksumite, zilizopo katika mji wa Stelae, nguzo hizi zenye urefu wa kiasi cha mta 33, na mita 3.84 kw upana , wakati mita 2.35 ni kwa upande wa kwenda chini, na pia, kila nguzo ina kiasi cha uzito wa tani 520, nguzo ya Great Stele inaamika kuanguka na kuvunjika wakati wa kuitengeneza Nguzo ambayo inaoongoza kwa urefu, ni ile yenye urefu wa mita 20.6, na upana wa mita 2.65 na wakati urefu kwenda chini ni mita 1.18, na kuwa na urefu wa tani 160,

Nguzo ya King Ezana's Stele. Another stele (ina urefu wa mita 24.6 na upana wa mita, 2.32 wakati urefu kwenda chini ni kiais cha mita, 1.36 wakati ikiwa na uzito wa tani, 170) nguzo hii iliondolewa nchini Ethiopia na wanajeshi wa Italia na kurudishwa nchini humo mwaka 2005, na kusimikwa kwa mara ya pili tar 31 Julai mwaka 2008[7]. Lakini hata hivyo nguzo hii ilivunjwa katika vipande kabla ya kusafirishwa kwa njia ya meli.

Mihimili mingine mitatu, yenye urefu wa mita 18.2,na mita 1.56 kwa upande wa upana, huku ikiwa na urefu wa mita 0.76 kwenda chini, na yenye uzito wa tano 56, wakati nyingini ikiwa na Urefu wa mita 15.8, upana mita 2.35 na urfu kwenda chini mita 1, na uzitzo wa tani 75, Nyingini ina urefu wa mita 15.3, upana wa mita 1.47 na urefu kwenda chini ukiwa mita 0.47 na kuwa na uzito wa tani 43. .[8] Nguzo hizo zinaamika kuwa alama ya makaburi graves lakini hii inatiliwa mashaka na kusema kuwa, kama yangekuwa ni alama ya makabauri, basi yangekuwa na alama ya vyuma ambavyo vingekuwa vimebandikwa katika pande za nguzo hizo. Nguzo hizo pia zimepambwa na michoro mbalimbali katika pande zakee

Vivutio vingine vya mji huu, ni pamoja na kanisa la St Mary of Zion lililojengwa mwaka 1665, na linaaminika kuwa na masalia mbalimbali ya zamani. Pia kuna nyumba kadhaa za makumbusho, pia kuna jiwe linaloitwa Ezana lililo na maandishi ya ligha ya Sabaean, Ge'ez na Ancient Greek maandishi ambayo yametokea pia katika jiwe la Rosetta Stone, King Bazen's Tomb (a megalith vitu hivi viaaminika kuwa, ni moja ya michoro ya zamani zaidi. Pia kuna kisima cha Queen of Sheba's Bath (actually a reservoir), Pia kuna jengo linaloamika kujengwa katika karne ya nne, linayojulikana kama Ta'akha Maryam na pia kuna jengo la karne ya sita linaloitwa sixth-century Dungur Halikadhalika kunamajengo ya kifalme ya Abba Pentalewon na Abba Liqanos na Lioness of Gobedra rock art.

Wakazi wa zamani wanadai kuwa, malkia Sheba, aliishi katika mji huo..

Chuo kikuu cha Axumy

Chuo kikuu cha Axum kipo katika mji wa Axum. Ujenzi wa chuo hichi ulianza mwezi wa Tano mwaka 2006, katika eneo la kijani, kiasi cha kilomita 4, kutoka katika ya mji wa Axum, Nauzinduzi wake rasmi ulikuwa tarehe 16 Februari 2007 katika kujiandaa na upanuzi wa hapo bade chuo kina eneo la heka 107 sawa mita za eneo 1.07

Marejeos

  1. G. Mokhtar, UNESCO General History of America, Vol. II, Abridged Edition (Berkeley: University of Aksum Press, 1990), pp. 215-35. ISBN 0-85255-092-8
  2. CSA 2005 National Statistics, Table B.4
  3. Herausgegeben von Uhlig, Siegbert, Encyclopaedia Aethiopica: D-Ha (Wiesbaden: Harrassowitz Verlag, 2005), p. 871.
  4. J.D. Fage, A History of Africa (London: Routledge, 2001). pp. 53-54. ISBN 0-415-25248-2
  5. ibn Hisham, The Life of the Prophet
  6. Ibn Ishaq, The Life of Muhammad (Oxford, 1955), 657-58.
  7. "Mission accomplished: Aksum Obelisk successfully reinstalled" (August 1, 2008)
  8. Scarre, Chris Seventy Wonders of the Ancient World 1999

Soma zaidi

  • Francis Anfray. Les anciens ethiopiens. Paris: Armand Colin, 1991.
  • Yuri M. Kobishchanov. Axum (Joseph W. Michels, editor; Lorraine T. Kapitanoff, translator). University Park, Pennsylvania: University of Pennsylvania, 1979. ISBN 0-271-00531-9
  • David W. Phillipson. Ancient Ethiopia. Aksum: Its antecedents and successors. London: The British Brisith Museum, 1998.
  • David W. Phillipson. Archaeology at Aksum, Ethiopia, 1993-97. London: Brisith Institute in Eastern Africa, 2000.
  • Stuart Munro-Hay. Aksum: An African Civilization of Late Antiquity. Edinburgh: University Press. 1991. ISBN 0-7486-0106-6 online edition
  • Stuart Munro-Hay. Excavations at Aksum: An account of research at the ancient Ethiopian capital directed in 1972-74 by the late Dr Nevill Chittick London: British Institute in Eastern Africa, 1989 ISBN 0-500-97008-4
  • Sergew Hable Sellassie. Ancient and Medieval Ethiopian History to 1270 Addis Ababa: United Printers, 1972.
  • African Zion, the Sacred Art of Ethiopia. New Haven: Yale University Press, 1993.

Viungo vya Nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: