Nenda kwa yaliyomo

Oti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Avena sativa)
Oti
(Avena sativa)
Oti
Oti
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Planta (mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Monocots (Mimea ambayo mche wao una jani moja tu)
(bila tabaka): Commelinids (Mimea kama kongwe)
Oda: Poales (Mimea kama nyasi)
Familia: Poaceae (Mimea iliyo na mnasaba na nyasi)
Jenasi: Avena
Spishi: A. sativa
L.
Kilimo cha oti duniani mwaka 2005
Punje za oti

Oti (kutoka Kiing. "oats") [1] ni mmea wa familia ya manyasi katika ngeli ya monokotiledoni. Mbegu au punje za oti ni nafaka ambayo ni chakula cha wanyama na pia cha watu katika nchi hasa za Ulaya na pia penginepo nje ya kanda ya tropiki. Tofauti na nafaka nyingi punje zake hazikai pamoja katika mshikano lakini ua lake linafanana zaidi na mpunga lakini mbegu ni tofauti kabisa.

Kihistoria ilikuwa chakula muhimu cha watu wa nchi za kaskazini kwa sababu inavumilia hali ya hewa baridi kiasi na mvua nyingi tofauti na ngano. Waroma waliona Wagermanik wa Kale walikula hasa oti; kwenye kisiwa cha Britania Waskoti hupenda oti lakini Waingereza hulisha nafaka hii kwa wanyama hasa farasi. Kupunguka kwa farasi kama wanyama wa kazi kwenye kilimo kumemaaanisha pia kurudi nyuma kwa kilimo cha oti.

Matumizi yake kwa binadamu ni katika uji, muesli, mkate na keki. Hutazamiwa kama chakula cha kujenga afya kutokana na wanga, vitamini na proteini ndaniy ake.

  1. Kamusi ya TUKI-ESD inataja "oats" kuwa "shayiri"; lakini shayiri ni "barley" jinsi inavyoonekana katika asili ya Kiarabu ya shayiri = شعير ambayo ni "barley"; linganisha pia kamusi za M-J SSE na Velten zinazotaja shayiri kuwa "barley / Gerste". "Oat" kwa Kiarabu ni شوفان shufan lakini haikuingia katika Kiswahili kwa sababu nafaka haistawi katika mazingira ya joto.
    Kamusi ya Kijerumani-Kiswahili ya Legere inatumia "oti" (Hafer). Labda asili ya kosa upande wa TUKI ni maelezo katika KKK/ESD: "oats - nafaka kama shayiri"
Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Oti kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.