Augusto Chapdelaine

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Augustino Chapdelaine)
Mt. Auguste Chapdelaine.

Augusto Chapdelaine, M.E.P. (La Rochelle, 6 Februari 1814Xilin, 29 Februari 1856) alikuwa padri kutoka Ufaransa aliyefanya umisionari barani Asia akauawa nchini China pamoja na Wakristo wapya wengi kwa ajili ya imani yake ya Kikristo[1] aliyekuwa wa kwanza kuieneza katika eneo la Guangxi.

Alipokamatwa alipigwa viboko mara 300, halafu akafungwa tunduni na mwisho alikatwa kichwa chake.

Alitangazwa kuwa mtakatifu pamoja na wengine 119 waliofuata kifodini chake na Papa Yohane Paulo II tarehe 1 Oktoba 2000.[2]

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake, lakini pamoja na wenzake ni tarehe 9 Julai[3].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. "Saint Francis Ferdinand de Capillas". Patron Saints Index. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-05-06. Iliwekwa mnamo 2008-04-24. 
  2. "Den hellige Frans Fernández de Capillas (1607-1648)" (kwa Norwegian). katolsk.no. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-02-09. Iliwekwa mnamo 2009-04-24. 
  3. Martyrologium Romanum
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.