Augustine Obiora Akubeze
Mandhari
Augustine Obiora Akubeze (alizaliwa Kaduna, Nigeria, 1956) ni kiongozi wa Kanisa Katoliki kutoka Nigeria na anahudumu kama askofu mkuu wa Jimbo Kuu la Benin City tangu mwaka 2011.
Tarehe 18 Machi 2011, Huduma ya Habari ya Vatikani iliripoti kuwa Papa Benedikto XVI alimteua Askofu Augustine Obiora Akubeze, wa Jimbo Katoliki la Uromi, Nigeria, kuwa askofu mkuu wa Jimbo Kuu la Benin City, Nigeria, kuanzia tarehe 28 Machi 2011.
Alipata daraja ya upadri mwaka 1987 na kisha akawekwa wakfu kuwa askofu mwaka 2006.[1]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ vanguard (2011-04-28). "New Archbishop installed at Benin Archdiocese of Catholic Church". Vanguard News (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2022-08-12.
| Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |