Nenda kwa yaliyomo

Auguste Escoffier

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Georges Auguste Escoffier (fr; 28 Oktoba 1846 – 12 Februari 1935) alikuwa Mfaransa mpishi, mmiliki wa mikahawa (restaurateur) na mwandishi wa sanaa ya upishi. Alisaidia kueneza na kuboresha mbinu za jadi za mapishi ya Kifaransa.

Mengi ya mbinu zake yalitokana na kazi za Marie-Antoine Carême, mmoja wa walioweka misingi ya haute cuisine ya Kifaransa. Mafanikio ya Escoffier yalikuwa kurahisisha na kuleta upya mtindo wa Carême ambao ulikuwa mgumu na wenye mapambo mengi. Hasa, alisanifisha (kudhibiti) mapishi ya kile kinachoitwa mother sauces tano.

Alijulikana na vyombo vya habari vya Ufaransa kama *roi des cuisiniers et cuisinier des rois* (“mfalme wa wapishi na mpishi wa wafalme”), jina ambalo pia lilikuwa limetumiwa awali kumuelezea Carême.[1] Escoffier alikuwa miongoni mwa watu mashuhuri sana katika London na Paris kuanzia miaka ya 1890 hadi mwanzoni mwa karne ya 20.

  1. Claiborne, Craig & Franey, Pierre. Classic French Cooking
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Auguste Escoffier kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.