Atang Tshikare
Atang Tshikare alizaliwa mwaka 1980 [1]ni msanii na mbunifu kutoka Afrika Kusini. Kazi zake zinashughulikia mada zinazohusiana [2]na ngano za jadi na urithi wa Watswana, huku akichunguza uhusiano kati ya ufundi wa jadi na teknolojia. Mara nyingi hutumia lugha ya usanifu wa kienyeji, zoomofia (umbo la wanyama), biomofia (umbo la viumbe hai), na mandhari ya Afrika.[3]
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Tshikare alizaliwa mjini Bloemfontein, Afrika Kusini mwaka 1980. Baba yake alikuwa mwanaharakati dhidi ya mfumo wa ubaguzi wa rangi (Apartheid) na mchoraji wa vielelezo.[4]
Anaishi na kufanya kazi mjini Cape Town. Utendaji wake wa kisanaa unahusisha nyanja za ufundi, ubunifu, na sanaa za maonesho (fine art).[Amefanya kazi kwa kutumia vifaa kama shaba (bronze), kauri, mawe, na mbao, na amechunguza mbinu za jadi za ufundi, pamoja na uundaji changamano wa kidijitali, akichanganya mbinu za kuiga haraka (rapid prototyping) na teknolojia za uchapishaji wa 3D[5]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.si.edu/object/atang-tshikare-1980-folder:SILAF_106940
- ↑ https://www.artmile.co.za/atang-tshikare
- ↑ https://africa.harvard.edu/news/atang-tshikare-south-african-artist-visits-harvard-center-african-studies
- ↑ "Atang Tshikare and the art of storytelling through design | Salone del Mobile". www.salonemilano.it (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2026-01-31.
- ↑ "Atang Tshikare and the art of storytelling through design | Salone del Mobile". www.salonemilano.it (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2026-01-31.
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Atang Tshikare kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |